Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 5, 2016

Mji wa Medina washambuliwa

Mripuko mkubwa umetokea katika mji wa Medina nchini Saudi Arabia.shuhuda wa tukio hilo anaeleza kwamba mtu aliyejitoa muhanga alifyatua kitufe cha kujilipulia karibu na msikiti mkubwa wa mtume, ambapo msikiti huo ni mmoja wapo ya eneo takatifu kwa waislamu.

Kituo cha runinga mjini Saudia kilionesha picha za moto mkubwa uliokuwa ukiwaka kwenye maegesho ya magari huku magari yakiteketea na mwili mmoja wa binaadamu ulionekana karibu yake.
Mpaka sasa hakuna kauli yoyote iliyotolewa na serikali ya Saudi Arabia kuhusiana na tukio hilo.tukio hili limetokea huku mtu mwingine wa kujitoa muhanga akiwa amejiripua katika msikiti wa madhehebu ya Shia upande wa Mashariki mwa mji wa Qatif, na mripuko wa tatu umetokea karibu na ubalozi wa Marekani mjini Jeddah.
Askari wawili wa kulinda usalama wamejeruhiwa katika mojawapo ya matukio hayo.na hakuna taarifa zozote kuhusiana na kundi lililo husika kupanga na kutekeleza mashambulizi hayo kuwa ni akina nani.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP