Baada ya wimbo wao uitwao Chausiku kufanya vizuri sokoni, Wasanii Payus (kushoto) na Mecrass (kulia) kutoka Jijini Mwanza ambao wanaunda kundi la Wapancrass, nyota yao imezidi kung'ara zaidi katika muziki.


Wasanii hao wamesema kwamba idadi ya wasanii wengine wanaoomba kufanya nao kazi imeongezeka tangu waachie wimbo wao wa Chausiku na kwamba hiyo ni ishara nzuri kuwa walichokifanya katika wimbo huo kimepokelewa vizuri.

"Baada ya kuombwa "collabo" na wasanii tofauti tofauti, tumeamua kuitikia wito. Kabla ya kuachia wimbo wetu mwaka huu, tutasikika katika wimbo ambao tumeshirikishwa na msanii Dumuz ambae pia anaiwakilisha vyema Kanda ya Ziwa". Amesema Mecrass na kuongeza kuwa wimbo huo ambao unafahamika kwa jina la "Umeniacha Mtupu" unatarajiwa kuingia sokoni Julai 25 mwaka huu.
Cover ya wimbo huo ambao unatarajiwa kutoka rasmi Julai 25 mwaka huu.
Imeandaliwa na BMG