Rais Obama wa Marekani amesema mauaji ya kikatili ya watu wawili weusi raia wa Marekani yaliyofanywa na polisi kama mengine yaliyotokea tukio jipya ni jambo kila Mmarekani anapaswa kulichukia.Rais Obama amesema ubaguzi umesababisha imani ya jamii kupungua dhidi ya polisi.

Katika picha video ya hivi karibuni inayomwesha marehemu Philando Castile akivuja damu ndani ya gari huku akinyoonyewa bunduki na polisi liliwekwa na rafiki yake wa kike kwenye mitandao ya kijamii.
Gavana wa Jimbo la Minisota Mark Dayton amesema hafikirii polisi waliompiga risasi na kumuua dereva huyo ambaye baadae walimvuta na kuvunja taa za mbele kama dereva huyo angekuwa mzungu.
Amesema atahakikisha uchanguzi wa tukio hilo ufanyika.Ninaaahidi nitafanya kila liwezekanavyo utawala pia utafanya kila linalowezekana ndani ya mamlaka yetu kukamilisha uchunguzi na kama ulivyosema mbele ya Robert Heron, haki lazima iheshimiwe.Haki lazima iheshimiwe Minesota. Haki lazima iheshimiwe.
Wakati wa maandamano hayo rafiki wa kike wa marehemu alielezwa kwa uchungu kile kilichotokea kwa rafiki yake aliyeuawa." Haikuwa risasi moja, hazikuwa mbili,hazikuwa tatu, hazikuwa nne zilikuwa risasi tano. Bila sababu. Inawezekanaje mtu kuweka mikono yake angani na kutoa kitambulisho kwa wakati mmoja wakati wanapokueleza kwamba alikuwa na silaha. Alipata wakati mgumu. Ilikuwa kwenye mfuko wa bastola kwenye suruali wakati walipomvuta kutoka kwenye gari wakati waleti yake ilipokuwa katika mfuko wa nyuma. Hawakutoa muda kwenye tukio hilo. Hawakuhakikisha anapumua. Harakaharaka walimtoa mwenzao pembeni walikamfariji. Mahali alipoanza kupiga kelele na kulia Ooh Mungu wangu siamini hili."