Rais Dkt John Magufuli
RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara ambao umeonesha kugusa kada tofauti za watu kutoka taasisi mbalimbali.
Uteuzi huo ulitangazwa jana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mussa Iyombe huku kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 ni wa zamani na 120 ni wapya.

Uteuzi huo unakamilisha serikali ambayo alianza kuiunda tangu Novemba mwaka jana wakati alipoteua mawaziri na manaibu wake, kisha akateua makatibu wakuu kabla ya kuteua wakuu wa mikoa Machi mwaka huu.
Aidha, baada ya uteuzi wa wakuu wa mikoa aliteua makatibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu tawala wa wilaya na kisha kumalizia na wakurugenzi hao aliowateua jana.
Katika uteuzi huo, mkurugenzi maarufu nchini ambaye ametumikia katika halmashauri mbalimbali nchini, Siporah Liana amekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo taarifa ya Ikulu iliyotolewa baadaye, inaonesha rais ameondoa katika orodha ya wakurugenzi hao wapya jina la Dk Leonard Masale ambaye alitajwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kumfanya mteule huyo kuendelea kufanya kazi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, kazi aliyopangiwa hivi karibuni.
Kutokana na mabadiliko hayo, nafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma itabakia wazi kusubiri uteuzi utakaofanywa baadaye. Miongoni mwa taasisi ambazo wafanyakazi wake wameteuliwa ni Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya HabariLeo, HabariLeo Jumapili, Daily News, Sunday News na SpotiLeo.
Mhasibu katika kampuni hiyo, Shafii Mpenda ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi cha Raawu (TSN), amepangiwa halmashauri ya Madaba mkoa wa Ruvuma. Aidha, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, Simon Berege ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari ameteuliwa kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
Mwandishi mwandamizi mwingine aliyeteuliwa ni Mhariri wa televisheni inayomilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mlimani Tv, Hamis Dambaya, anayekwenda Wilaya ya Nanyumbu. Ndani ya uteuzi huo, yumo wakili wa jijini Dar es Salaam Elias Nawela, aliyepangiwa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.
Uteuzi mara mbili
Wakati huo huo, Ikulu imefafanua kuwa makatibu tawala wa wilaya wote ambao majina yao yamejitokeza katika orodha ya wakurugenzi wa halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na wilaya, Rais Magufuli ameamua kuwabadilishia majukumu na sasa watatumikia vyeo vyao vya ukurugenzi badala ya vyeo vya Ukatibu Tawala wa Wilaya.
Kutokana na mabadiliko hayo, nafasi za Makatibu Tawala wa Wilaya ambao wameteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri zitajazwa baadaye. Taarifa hiyo ya Ikulu ilisema wakurugenzi wote walioteuliwa wanatakiwa kufika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Jumanne Julai 12, saa tatu asubuhi kwa ajili ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.
Orodha kamili ya wakurugenzi walioteuliwa kulingana na mikoa yao ni kama ifuatavyo;
ARUSHA
Arusha Jiji -Athumani Juma Kihamia
Arusha DC - Dk Wilson Mahera Charles
Karatu DC - Banda Kamwande Sonoko
Longido DC - Jumaa Mohamed Mhiwapijei
Meru DC - Kazeri Christopher Japhet
Monduli DC - Stephen Anderson Ulaya
Ngorongoro DC - Raphael John Siumbu
DAR ES SALAAM
Dar es Salaam Jiji - Siporah Jonathan Liana
Kinondoni Manispaa - Aron Titus Kagurumjuli
Temeke Manispaa - Nassibu Bakari Mmbaga
Ilala Manispaa - Msongela Nitu Palela
Kigamboni Manispaa - Stephen Edward Katemba
Ubungo Manispaa - Kayombo Lipesi John
DODOMA
Dodoma Manispaa - Dk Leonard M. Masale
Kondoa DC - Kibasa Falesy Mohamed
Kondoa Mji - Khalifa Kondo Mponda
Mpwapwa DC - Mohamed Ahamed Maje
Kongwa DC - Mhandisi Ngusa Laurent Izengo
Chemba DC - Semistatus Hussein Mashimba
Chamwino DC - Athuman Hamis Masasi
Bahi DC - Rachel Marcel Chuwa
GEITA
Bukombe DC - Dionis Maternus Nyinga
Chato DC - Mhandisi Joel Bahahari
Geita DC - Ally Abdallah Kidwaka
Geita Mji - Modest J. Apolinaly
Mbogwe DC - Mahwago Elias Kayandabila
Nyang’wale DC - Carlos K. Gwamagobe
IRINGA Iringa
Manispaa - William Donald Mafwele
Mafinga Mji - Saada S. Mwaruka
Mufindi DC - Riziki Salas Shemdoe
Iringa DC - Robert Mgendi Magunya
Kilolo DC - Aloyce Kwezi
KAGERA
Biharamulo DC - Wende Israel Ng’ahala
Bukoba DC - Abdulaaziz Jaad Hussein
Bukoba Manispaa - Makonda Kelvin Stephen
Karagwe DC - Godwin Moses Kitonka
Kyerwa DC - Shedrack M. Mhagama
Missenyi DC - Limbe Berbad Maurice
Muleba DC - Emmanuel Shelembi Luponya
Ngara DC - Aidan John Bahama
KATAVI
Mlele DC - Alex Revocatus Kagunze
Mpimbwe DC - Erasto Nehemia Kiwale
Mpanda DC - Ngalinda Hawamu Ahmada
Mpanda Manispaa - Michael Francis Nzyungu
Nsimbo DC - Joachim Jimmy Nchunda
KIGOMA
Buhigwe DC - Anosta Lazaro Nyamoga
Kakonko DC - Lusubilo Joel Mwakabibi
Kasulu DC - Godfrey Msongwe Masekenya
Kasulu Mji - Fatina Hussein Laay
Kigoma Ujiji - Manispaa - Judethadeus Joseph Mboya
Kigoma DC - Hanji Yusuf Godigodi
Kibondo DC - Shelembi Felician Manolo
Uvinza DC - Weja Lutobola Ng’olo
KILIMANJARO
Manispaa ya Moshi - Michael Nelson Mwandezi
Hai DC - Yohana Elia Sintoo
Siha DC - Valerian Mwargwe Juwal
Same DC - Shija Anaclaire
Mwanga DC - Golden A. Mgonzo
Rombo DC - Magreth Longino John
Moshi DC - Emalieza Sekwao Chilemeji
LINDI Kilwa DC - Bugingo I. N. Zabron
Lindi DC - Samwel Warioba Gunzar
Lindi Manispaa - Jomaary Mrisho Satura
Liwale DC - Justine Joseph Monko
Nachingwea DC - Bakari Mohamed Bakari
Ruangwa DC - Andrea Godfrey Chezue
MANYARA
Babati Mji - Fortunatus Hilario Fwema
Hanang DC - Bryceson Paul Kibasa
Mbulu DC - Festi Fungameza Fwema
Mbulu Mji - Anna Philip Mbogo
Simanjiro DC - Yefred Edson Myezi
Kiteto DC - Tamim Kambona
Babati DC - Hamis Iddi Malinga
MARA
Manispaa ya Musoma - Fidelica Gabriel Myovela
Bunda DC - Amos Jeremiah Kusaja
Bunda Mji - Janeth Peter Mayanja
Butiama DC - Solomon Kamlule Ngiliule
Musoma DC - Flora Rajab Yongolo
Serengeti DC - Juma Hamsini Seph
Rorya DC - Charles Kitanuru Chacha
Tarime DC - Apoo Castro Tindwa
Tarime Mji - Hidaya Adam Usanga
MBEYA
Busokelo DC - Eston Paul Ngilangwa
Chunya DC - Sofia Kumbuli
Kyela DC - Mussa Joseph Mgata
Mbarali DC - Kivuma Hamis Msangi
Mbeya DC - Ameichiory Biyengo Josephat
Mbeya Jiji - Zacharia Nachoa Ntandu
Rungwe DC - Loema Isaya Peter
SONGWE
Momba DC - Adrian Jovin Jungu
Tunduma Mji - Valery Alberth Kwemba
Mbozi DC - Edna Amulike Mwaigomole
Ileje DC - Haji Mussa Mnasi
Songwe DC - Elias Philemon Nawela
MOROGORO
Gairo DC - Agnes Martin Mkandya
Kilombero DC - Dennis Lazaro Londo
Ifakara Mji - Francis Kumba Ndulane
Kilosa DC - Kessy Juma Mkambala
Morogoro DC - Sudi Mussa Mpili
Morogoro Manispaa - John Kulwa Magalula
Mvomero DC - Florent Laurent Kyombo
Ulanga DC - Audax Christian Rukonge
Malinyi DC - Marcelin Rafael Ndimbwa
MTWARA
Mtwara DC - Omari Juma Kipanga
Mtwara Mikindani Manispaa - Beatrice Dominic Kwai
Masasi Mji - Gimbana Emmanuel Ntayo
Masasi DC - Mkwazu M. Changwa
Nanyumbu DC - Hamis Hassan Dambaya
Newala DC - Mussa Mohamed Chimae
Newala Mji - Andrew Frank Mgaya
Tandahimba DC - Said Ally Msomoka
Nanyamba Mji - Oscar Anatory Ng’itu
MWANZA
Mwanza Jiji - Kiomoni Kibamba Kiburwa
Ilemela Manispaa - John Paul Wanga
Kwimba DC - Pendo Anangisye Malabeja
Magu DC - Lutengano George Mwalwiba
Misungwi DC - Eliud Leonard Mwaiteleke
Ukerewe DC - Tumaini Sekwa Shija
Buchosa DC - Crispian Methew Luanda
Sengerema DC - Magesa M. Boniphace
NJOMBE
Njombe Mji - Iluminata Leonald Mwenda
Makambako Mji - Paul Sostenes Malala
Makete DC - Francis Emmanuel Namaumbo
Njombe DC - Monica Peter Kwiluhya
Ludewa DC - Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija
Wanging’ombe DC - Amina Mohamed Kiwanuka
PWANI
Bagamoyo DC - Azimina A. Mbilinyi
Chalinze DC - Edes Philip Lukoa
Kibaha DC - Tatu Seleman Kikwete
Kibaha Mji - Jenifer Christian Omolo
Kisarawe DC - Mussa L. Gama
Mafia DC - Erick Mapunda
Mkuranga DC - Mshamu Ally Munde
Kibiti DC - Alvera Kigongo Ndabagoye
Rufiji DC - Salum Rashid Salum
RUKWA
Kalambo DC - Simon Ngagani Lyamubo
Sumbawanga DC - Nyangi John Msemakweli
Sumbawanga Manispaa - Hamid Ahmed Njovu
Nkasi DC - Julius M. Kaondo
RUVUMA
Mbinga DC - Gumbo Samanditu Gumbo
Mbinga Mji - Robert Kadaso Mageni
Namtumbo DC - Christopher Michael Kilungu
Nyasa DC - Oscar Albano Mbuzi
Songea DC - Simon Michael Bulenganija
Madaba DC - Shafi Kassim Mpenda
Tunduru DC - Abdallah Hussein Mussa
Songea Manispaa - Tina Emelye Sekambo
SHINYANGA
Kishapu DC - Stephen Murimi Magoiga
Msalala DC - Berege Sales Simon
Shinyanga
DC - Mark Emmanuel Malembeka
Kahama Mji - Anderson David Msumba
Shinyanga Manispaa - Lewis Kweyemba Kalinjuna
Ushetu DC - Michael Augustino Matomola
SIMIYU
Bariadi DC - Abdallah Mohamed Malela
Bariadi Mji - Melkizedek Oscar Humbe
Itilima DC - Mariano Manyingu
Maswa DC - Fredrick Damas Sagamiko
Busega DC - Anderson Njiginya
Meatu DC - Said F. Manoza
SINGIDA
Ikungi DC - Rustika William Turuka
Iramba DC - Linno Pius Mwageni
Mkalama DC - Martin Msuha Mtanda
Manyoni DC - Charles Edward Fussi
Itigi DC - Luhende Pius Gerald
Singida DC - Rashid Mohamed Mandoa
Singida Manispaa - Kizito L. Brava
TABORA
Igunga DC - Revocatus Lubigili Kuuli
Kaliua DC - John Marco Pima
Nzega DC - Jacob James Mtalitinya
Nzega Mji - Phillimon Mwita Magesa
Sikonge DC - Simon Saulo Ngatunga
Tabora Manispaa - Bosco Addo Ndunguru
Urambo DC - Magreth Nakainga
Tabora -Uyui - Hadija Maulid Makuani
TANGA
Tanga Jiji - Daudi R. Mayeji
Korogwe DC - George John Nyaronga
Korogwe Mji - Jumanne Kiangoshauri
Muheza DC - Luiza Osmin Mlelwa
Handeni Mji - Keneth K. Haule
Handeni DC - William Methew Mafukwe
Pangani DC - Sabas Damian Chambasi
Mkinga DC - Mkumbo Emmanuel Barnabas
Bumbuli DC - Peter Isaiah Nyalali
Kilindi DC - Clemence Andagile Mwakasenda
Lushoto DC - Kazimbaya Makwega Adeladius.