Taasisi ya saratani ya Uganda imetia saini na hospitali ya Aga Khan yanairobi Kenya kutoa mwanya kwa wagonjwa wa saratani wa Uganda kuweza kupata matibabu ya kutu mitambo ya Redio therapi. Hii inafuatia mtambo kama hupo wa hospitali kuu ya Uganda ya Mulago kuharibika na kuwaacha wagonjwa kubaki bila tiba jambo ambalo lilipelekea baadhi kufariki.
Mapatano kati ya hospitali ya Aga Khan ya Nairobi na taasisi ya saratani ya Uganda yamefikiwa kufuatia mazungumzo ya muda mrefu.Taarifa iliotolewa na taasisi ya saratani pamoja na hospitali ya aga Khan kwa pamoja inasema kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kuwapa mataibabu ya mitambo ya redio -therapi wagonjwa wa uganda takriban 400 tena kwa bure.
Hati ya makubaliano imetiwa sahihi na vigogo kutoa sehemu mbili husina.Upande wa Uganda umeongozwa na katibu mkuu wa wizara ya afya ya Uganda Bw Ronald Segawa akiwa na Dr Jackson Orem mkurugenzi wa taasisi ya saratani ya Uganda pamoja na balozi wa Amin Mawji mjumbe wa kibalozi na vigogo kadhaa.


Miezi kadhaa iliopita wakati mashine redio thrapi ilipoharibika na kuwaacha wagonjwa takriban 400 kuchanyikiwa Katibu wa kudumu wa wizara ya afya Dr Asuman Lukwago..aliiarifu BBC kuhusu mpango huo.Hata hivyo tangu wakati huo hakuna hata mgonjwa mmoja wa Uganda aliepelekwa Nairobi huenda kulikuwa na shughuli ambazo ziltakiwa kutatuliwa kwanza ndio hayo mazungumzo.
Katika taarifa iliotolewa inamunukuu Dr Orem wa taasisi ya saratani akisema kuwa wamefurahia makubaliano haya kwani vizuizi karibu vyote vilivyokuwa vinakingama mpango huo, kama vile masuala ya kiutawala na kifedha yametatuliwa bada ya mapatano hayo.
Gharama za matibabu zitasimaiwa na mpango wa ustawi wa hospitali ya chuo kikuu cha Aga Khan ya Nairobi