Afrika kusini ndiyo yenye uchumi mkubwa Afrika .Kwa miaka mwili iliyopita, Nigeria ilidai kuwa kileleni, lakini mahesabu mapya ya matumizi ya viwango vya sarafu yameliweka taifa la Afrika Kusini tena kileleni.

Mahesabu mapya yanazingatia kiwango vya shirika la fedha la kimataifa(IMF) vya tarakimu za pato la jumla la ndani ya nchi kwa nchi zote mbili katika mwaka 2015.
Katika kipindi cha mwaka huu kufikia sasa, randi ya Afrika kusini na naira ya Nigeria zimekua na mwelekeo tofauti dhidi ya dola. Thamani ya randi iliongezeka kwa takriban asilimia 16%, huku naira ikipoteza robo ya thamani yake dhidi ya dola ya Marekani.
Lakini hakuna cha mno sana - kwani kwa dola bilioni 301 Afrika kusini imeipiku Nigeria kwa dola bilioni 5 tu.
Uchumi wa mataifa hayo mawili uko katika hatari ya kuanguka katika msuko suko kutokana na kwamba uchumi wa mataifa haya mawili ulididimia katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu