Mtu mmoja aliyejaribu kupanda mnara wa Trump uliopo jijini New York, ameondolewa na polisi katika jengo hilo baada ya kuchomwa na vioo vya jengo hilo lenye ghorofa hamsini na nane ambayo ni makao makuu ya kampeni za kumchagua Donald Trump.

Mpandaji alionekana amelewa
Image captionMpandaji alionekana amelewa

Trump anaishi kwenye chumba cha juu ya ghorofa hilo lakini kwa sasa anafanya kampeni zake nje ya mji.
Mpandaji alijivuta huku akiwa akionekana kuwa amelewa, akitaka kuingia ndani ya jengo hilo.

Umati wa watu ukishuhudia polisi wakimuondoa
Image captionUmati wa watu ukishuhudia polisi wakimuondoa

Polisi waliofika eneo la tukio wamesema hawakuweza kutambua nini haswa lilikuwa lengo lake.

Hatimaye polisi walifanikiwa kumuingiza ndani ya jengo hilo
Image captionHatimaye polisi walifanikiwa kumuingiza ndani ya jengo hilo