Muanzilishi na Mkurugenzi
mtendaji wa Asasi ya
FEDHA Jafari Selemani akizungumzia changamoto za
vijana na watanzania kwaujumla juu
  ya kutokufikia
Uhuru wa kifedha (financial freedom) ikiwemo ukosefu wa
elimu ya usimamizi fedha binafsi ambapo inapelekea


umasikini wa
watanzania wengi, pia
alitumia nafasi hiyo kuzindua progranu ya
FEDHA KLABU ambayo itakayowapa fursa vijana kupata elimu ya udhibiti
fedha binafsi buree kila jumamosi chuoni hapo.


Ni mshauri wa vijana pia ni Meneja Masoko wa Taasisi ya  FEDHA Abdalah Kipinga akiongea na wanafunzi wa
chuo ch Kilimanjaro ambapo alizungumzia juu ya maisha ya wanavyuo na changamoto
zake na jinsi ya kuzikabili.

Mhamasishaji wa vijana Elly David akizungumza na wanafunzi
wa chuo cha Kilimanjaro (hawapo pichani)  ambapo alizungumza kuhusu siri ya mafanikio
kwa vijana na kuwaasa kusimamia ndoto zao lkatika kongamano lililofanyika
mwishoni wa wiki iliyopita chuoni hapo

Wanafunzi wa chuo cha kilimanjaro wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo lililowezeshwa na Taasisi ya Fedha mwsihoni wa wiki iliyopita

Baadhi ya  washiriki wa kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji katika kongamano hilo lilifnayika mwisho wa wiki iliyopita chuoni hapo Sinza Mapambano ,Jijini Dar es salaam.