Katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa Afrika Kusini, chama tawala cha ANC, kimeshindwa na Democratic Alliance, katika eneo lenye mji mkuu,Pretoria.
Matokeo ya mwisho ya eneo hilo la Tshwane, yanaonesha kuwa chama cha Democratic Alliance kimepata asilimia 43 ya kura na ANC asilimia 41.

Chama cha Democratic Alliance kitalazimika kuunda serikali ya mseto kuongeza udhibiti katika eneo.
Vyama viwili vikuu pia vinakaribiana kudhibiti Johannesburg, mji mkubwa kabisa nchini humo.
Matokeo ya mwisho yanatarajiwa saa moja jioni saa za Afrika Mashariki.
ANC imepata matokeo mabaya zaidi tangu kuingia madarakani, baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi kumalizika.