Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa taarifa juu ya kusimama kwa ujenzi wa Zahanati hiyo.


Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya ya ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri wakati akitoa maelezo wakati wa kikao cha serikali ya kijiji



Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali wakati wa ziara yake Wilayani humo

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

Umakini wa wananchi ukiwa umetawala wakati wa Mkutano wa Kijiji, Wilayani ikungi


Na Mathias Canal, Singida




Serikali ilitangaza eneo la Hifadhi ya msitu wa wananchi waliomo ndani
mwaka 2003 ambao kutangazwa huko kuliashiria wananchi kuhama katika
maeneo hayo ili kutoa fursa kwa serikali kusimamia kwa karibu eneo hilo
lakini wananchi hao mpaka sasa hawajahama kwa kukaidi agizo hilo.



Jambo hili limemsukuma Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
kufanya ziara na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo kwa lengo la
kuwaelemisha juu ya uvunjaji sheria za nchi kwa kuendelea kusalia katika
maeneo ambao wametakiwa kuhama jambo ambalo kama watashindwa
kulitekeleza serikali itawatoa kwa nguvu kwani kwa kiasi kikubwa
wanaharibu mazingira.



Akizungumza na Wananchi hao katika Kijiji
cha Kaugeri Kata ya Mwaru Wilayani hapa Dc Mtaturu ametoa mwezi mmoja
kwa wananchi hao kuhama haraka iwezekanavyo ili kupisha eneo hilo la
Hifadhi ya msitu kufanya Kazi iliyokusudiwa kwa zaidi ya miaka kumi
sasa.



Mtaturu amesema kuwa Kwa mujibu wa sheria Kijiji kinapaswa
kutoa Ardhi hekari zisizozidi hamsini kwa mwekezaji lakini uongozi wa
Kijiji hicho umegawa kwa mwekezaji hekta 150 hadi 200 kinyume kabisa na
taratibu za kiutendaji ukiwa ni pamoja na kuingia mikataba ya
kinyonyaji.



Pamoja na hayo pia viongozi hao wametoa Ardhi hiyo
bila kushirikisha wananchi jambo ambalo limeibua hisia Kali kwa wananchi
ambao wanatambua uporwaji huo wa maeneo yao.



Kufuatia kadhia
hiyo ya viongozi hao kugawaji Ardhi kinyume na taratibu Dc Mtaturu
amewaweka lumande Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri Mange Nkuba,
Aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Laurent Bomba, na mjumbe wa serikali ya
Kijiji Paul Kilo huku Amani Clement ambaye alitoweka kabla Ya mkutano
kumalizika anaendelea kutafutwa mpaka apatikane.



Katika hatua
nyingine Dc Mtaturu ameagiza mkandarasi Samwel John kukamatwa na
kuhojiwa kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji tangu
Mwaka 2013 ambapo tayari alishapewa kitita cha shilingi milioni 19 kwa
ajili ya kukamilisha ujenzi huo.



Hata hivyo pamoja na mkandarasi
kukabidhiwa fedha hizo alianza ujenzi lakini jengo hilo halijafika hata
kwenye Renta huku likiwa limejengwa chini kiwango.



Sambamba na
hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi amemuagiza mkurugenzi wa
Halamashauri ya Wilaya hiyo kupitia idara ya ujenzi kutoa taarifa
kwanini hawakushiriki kutoa huduma za kiutaalamu katika kusimamia jengo
hilo la umma kabla na wakati ujenzi unaanza.