Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akishiriki shughuli za maendeleo kwa kufyeka baadhi ya vichaka


 Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akizungumza na viongozi wa Kijiji na Kata ya Gonja Maore na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya







Dc Senyamule akishiriki zoezi la kupanga matofali yaliyofyatuliwa na wananchi wenyewe kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilayani humo.


Na Mathias Canal, Kilimanjaro



Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ametenga Siku moja katika Juma ili
kushiriki shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi.



Huu ni utaratibu ambao Mkuu huyo wa Wilaya ameuanzisha kwa muktadha wa
kuchochea ari katika utendaji Kazi na uwajibikani kwa kila mwananchi ili
kuimarisha na kusukuma kwa vitendo juhudi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa vitendo na utekelezaji wa utendaji
kazi ili kuakisi dhana nzima ya serikali hii ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu.



"Nimeamua kutenga siku hii ya jumatatu kwani naamini italeta hamasa kwa
wananchi kupenda kazi za maendeleo, itawatia moyo na kuona kuwa serikali ipo
karibu nao ". Alisema Staki



Akizungumzia kuhusu kuanza kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi Dc Staki amesema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanaoishi kwa
mazoea ya kuyumbishwa na siasa zisizo na manufaa kwao lakini huu si wakati tena
wa kurudi nyuma badala yake watanzania wote wanapaswa kushirikiana katika
kufanya Kazi na kulifanya Taifa Letu kufika mbali zaidi kimaendeleo.



Hii imekuwa ziara ya mwanzo ya Mkuu huyo wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki kwa kushiriki
kufanya kazi za Jamii akiwa na dhamira ya kuwatia Moyo wananchi ili kupunguza
lawama zisizo na lazima kwa serikali na badala yake kujituma katika kufanya
kazi.



Ziara hiyo katika kushiriki Kazi za jamii imefanyika katika kijiji cha Mheza
na Maore vilivyopo kata ya Gonja Maore huku wananchi wakijitokeza kwa wingi
kuishauri na kushirikiana na serikali.



Kwa upande wawananchi wa maeneo hayo walionyesha kufurahishwa na utaratibu
huo ambao haujawahi kufanyika na kiongozi yeyote katika Wilaya ya Same tangu
kuumbwa kwa msingi ya ulimwengu.



Wananchi hao wamemuakikishia Mkuu hiyo wa Wilaya hiyo kuwa watashirikiana
nae katika shughuli za maendeleo kwani kwa kiasi kikubwa udini na uzembe wa
watendaji wengi umesababisha kuendelea kuzorota kwa maendeleo ya Wilaya, Mkoa
na Taifa kwa ujumla.



Pamoja na hayo pia Dc Staki Ametoa
onyo kwa wananchi hususani Vijana ambao ni wavivu katika kushiriki shughuli za
Jamii kuchukuliwa hatua Kali za kinidhamu kW kila mwananchi atakayeshindwa
kutekeleza wajibu wake.