Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry ameitaka Sudan Kusini kuwakubali wanajeshi 4000 wa Umoja wa Mataifa nchini humo.
Akizungumza baada ya kukutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mawaziri wa maswala ya kigeni jijini Nairobi,Kerry amesema kuwa Sudan Kusini inafaa kuheshimu makubaliano ya amani nchini humo kwa maneno na vitendo ili kuhakikisha kuwa yanaafikiwa.
Amewataka viongozi wa taifa hilo kutojihusisha na vitendo vya ghasia ambavyo vinaweza kuchangia vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mapema mwezi huu Sudan Kusini ilisema kuwa haitashirikiana na Umoja wa Mataifa .

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Image captionRais wa Sudan Kusini Salva Kiir

Bwana Kerry pia amesema kuwa mafanikio makubwa yameafikiwa katika kukabiliiana na tishio la wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini Somalia,lakini mengi yanahitajika kufanywa katika eneo hili.
Ameongezea kuwa Marekani itaahidi dola milioni 138 za misaada ya kibinaadamu kwa Sudan Kusini mwaka huu.