Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akieleka ukumbi wa mkutano wakati wa kikao alichofanya na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani.Kushoto ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Abdulrahman Kaniki na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Askari Polisi hao ni wadau muhimu katika kufanikisha Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiwa amesimama wakati askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani(hwapo pichani), wakiimba wimbo wa maadili wa Jeshi la Polisi. Kushoto ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Abdulrahman Kaniki na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani(hawapo pichani) wakati wa mkutano na askari hao wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani(hawapo pichani) wakati wa mkutano na askari hao wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Edwin Ngonyani, akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani(hawapo pichani) wakati wa mkutano na askari hao wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, akiuliza swali wakati wa mkutano ambao mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) .Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, wakimsikiliza Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) wakiwa ni wadau muhimu katika Mkakati wa Baraza wa kukabiliana na ajali za barabarani nchini, uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. (Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)