Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
MAWAZIRI wa wizara mbalimbali, wanapaswa kuhamia Dodoma, ndani ya wiki tatu baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (pichani) kuhamia.
Waziri Mkuu alishatangaza kuwa atakuwa amehamia ifikapo Septemba, mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wa Idara ya Mazingira katika ofisi yake, wajipange vizuri kwa ajili ya kufanya tathmini ya athari za kimazingira mjini Dodoma wakati serikali ikijiandaa kuhamia kwenye mji huo.

Mawaziri hao ambao wameshatajwa kwa majina, wanapaswa kuhamia Dodoma ndani wiki mbili hadi tatu baada ya Majaliwa kuhamia Dodoma.
Agizo la watendaji wa serikali kutakiwa kuhamia Dodoma kwa awamu, lilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri huyo alisema hivi sasa mji wa Dodoma, unaweza kupokea serikali kwa asilimia 70 na kwa upande wa watumishi maandalizi yamekamilika kwa asilimia 75, hivyo kuhamia Dodoma inawezekana kwa sababu jambo hilo litafanywa kwa awamu.
Kutokana na taarifa hiyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba ambaye alishatangaza kuhamia Dodoma akiwa waziri wa kwanza kutoa kauli hiyo baada ya Waziri Mkuu, alisema jana kuwa wameshapokea maagizo. Tizeba alisema kwamba ndani ya wiki mbili hadi tatu, baada ya Waziri Mkuu kuhama, nao wanapaswa wawe wameshafika.
“Ni kweli awali nilisema nitaha - m i a Dodoma n d a n i ya wiki m o j a kuanzia siku nilipotangaza hilo, l a k i n i sikufanik i s h a , na hii ni kutokana na serikali kupitia Waziri Mhagama kuweka utaratibu wa kufuata kwa mawaziri kuhamia Dodoma,” alisema Dk Tizeba.
Alisema wao kama wizara, walishajipanga na kujiandaa kuhamia Dodoma na kwamba walichokuwa wanasubiri ni maelekezo ya kufuata katika kutekeleza agizo hilo la Rais John Magufuli.
Akizungumzia kuhusu watendaji na watumishi wa wizara hiyo kuhamia Dodoma, Dk Tizeba alisema kama ilivyotangazwa na Waziri Mhagama, kwamba serikali itahama kwa awamu, nao wameshapokea maelekezo ya kuhamia Dodoma, na kwamba kwa kuanza watakaokwenda ndani ya muda huo ni watendaji wakuu wa wizara.
“Tumeelekezwa tutahamia kwa awamu, ila sasa tunaopaswa kwenda ni watendaji wakuu wa wizara na baadaye tutaangalia uwezo wa mji wa Dodoma kupokea watumishi wengine, ila sisi wizara tumeshajipanga,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Kaimu Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, alisema wizara hiyo imejipanga kuhamia D o d o - ma na kwamba w a n a - c h o - subiri ni utekelezaji wa kwenda huko.
“ S i s i tumeshajiandaa na hata watumishi wa w i z a r a wanafahamu na w a m e - jiandaa, tunachosubiri ni maelekezo tu ya kuondoka,” alisema Mwaipaja.
Wakati wizara hizo mbili, zikiwa tayari kwa kuelekea Dodoma, nayo Wizara ya Nishati na Madini kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Profesa Justin Ntalikwa imesema maelekezo kwa wakuu wa idara na vitengo wote, yameshatolewa ili kufanya maandalizi kwa ajili ya kuhamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.
Akitangaza kuhamia Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ameshaagiza ukarabati kwenye nyumba yake, ukamilishwe ili ifikapo Septemba aweze kuhamia na kuwataka mawaziri kufanya hivyo kwa sababu kila Waziri ana nyumba na ofisi ndogo mjini Dodoma.
Hivi karibuni kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika mjini Dodoma, Rais John Magufuli alisisitiza azma ya serikali yake kuhamia Dodoma ndani ya miaka minne na nusu iliyobaki ya utawala wake.