Rais John Magufuli na mkewe Janet Magufuli ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria ibada ya Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya ndoa ya Rais Mstaafu awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe Anna Mkapa.

Misa ya maadhimisho hayo yaliyofanyika latika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay imeongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Policarp Kardinali Pengo na kuhudhuriwa na maaskofu na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi za umma.
Wageni maarufu waliohudhuria maadhimisho hayo pamoja na Mawaziri Wakuu wastaafu wa Tanzania Cleopa Msuya, Dk Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba, Edward Lowassa na mkewe na mjane wa baba wa taifa, mama Maria Nyerere.