Mkimbizi mmoja wa Syria Ninorta Bahno ameshida taji la 'Umalkia' na kampuni moja ya kutengeneza mvinyo Ujerumani . Ni mkimbizi wa kwanza kupokea tuzo hilo.
Ninorta Bahno, 26, mwanafunzi ameitoroka Syria zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
MSyria huyo mkristo alizawadia tuzo hilo huko mjini Trier, magharibi mwa Ujerumani, katika eneo la Moselle karibu na mpaka na Luxembourg , ambalo linajulikana sana kwa kutengeneza mvinyo.
Ninorta Bahno asema anatumai taji hilo litasaidia kuleta utengamano baina ya raia wa ujerumani na wakimbizi wanaotafuta hifadhi nchini humo kama yeye.
"Nataka kuonesha kwamba Ujerumani ni nchi inayopokea na kukaribisha wakimbizi na wanajitahidi katika kushughulikia maombi ya wanotafuta hifadhi haraka iwezekanavyo," Bi Bahno,amenukuliwa kusema akiendelea kusema "Kama mkimbizi ni vigumu sana kutangamana na watu katika nchi ya kigeni."

Hapa Ninorta Bahno aonekana akiwa na glasi ya mvinyo wa Riesling katika eneo la shamba la mimea ya kutengeneza mvinyo huko Trier, Ujerumani , 28 Juni 2016
Image captionNinorta Bahno atakuwa akisaidia katika kutangaza biashara hizo kwa niaba ya watengenezaji mvinyo wa eneo hilo

Mwaka jana Ujerumani ilipokea wakimbizi zaidi ya millioni moja igrants, wengi wao kutoka Syria.
Ms Bahno atakuwa akiwawakilisha watengezaji mvinyo wa eneo hilo katika tamasha mbalimbali za huko Trier.
Anasema baadhi ya wakimbizi aliozungumza nao wamefurahiya na kumpongeza kwa kushinda taji hilo.
Ms Bahno anasema ilimbidi kufanya mafunzo ya dharura ya jinsi ya kutengeneza mvinyo na anapendelea ule iitwayo sweet Riesling.
Taji hiyo la Malkia wa Ujerumani ilianza tangu 1930.
Mashindano hayo hufanyika kila Septemba, na majimbo 13 ya Ujerumani hushiriki kuwania taji hilo la 'The German Wine Queen'.