Mo Farah amekuwa mwanariadha wa kwanza wa Uingereza wa mbio na uwanjani kushinda nishani tatu za dhahabu katika michezo ya olimpiki, baada ya kuwaonyesha wakenya na waethiopia kivumbi, na kushinda mbio za mita 10,000 mjini Rio.
Mwanariadha huyo, aliye na umri wa miaka 33, alijikwaa wakati wa mbio hizo, japo alijikakamua vilivyo katika mita 100 za mwisho na kushinda kwa muda wa dakika 27 sekunde 5.
Mkenya Paul Tanui ameshinda nishani ya fedha, huku mwanariadha wa Ethiopia Tamirat Tola akimaliza wa tatu.
Farah atarejea uwanjani jumatano kutetea taji lake la mbio za mita 5,000, aliloshinda miaka minne iliyopita mjini London.
"Nimeshinda dhahabu tatu kwa wanangu watatu,," Farah alisema. "Ningetaka kushinda dhahabu ya nne katika mbio za mita 5,000 kwa mtoto wangu mchanga."
Iwapo atashinda mbio hiyo, ataafikia mafanikio sawa na ya mwanariadha wa Finland Lasse Viren aliyehifadhi mataji mawili ya olimpiki katika mbio za mwendo mrefu mwaka wa 1976.

Mwanariadha wa Finland Lasse VirenImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionMwanariadha wa Finland Lasse Viren aliyehifadhi mataji mawili ya olimpiki katika mbio za mwendo mrefu mwaka wa 1976.

Hata hivyo Mo Farah alipata ushindani mkubwa kutoka kwa Mkenya Paul Tanui, na ilimbidi atumie nguvu za ziada kuongoza mbio hizo.
Mwandishi wa BBC wa michezo Tom Fordyce anasema, "Mra ya mwisho kumwona Mo Farah akiwa nyuma katika fainali za mashindano makubwa, ni miaka mitano ilopita mjini Daegu"