Daktari mmoja wa tiba ya maungo amesema kuwa vijana wadogo wanahatarisha afya yao ya uzazi kwa kuangalia sana picha za ngono katika mitandao ya kijami.

Angela Gregory kutoka hospitali ya chuo kikuu cha Nottingham amesema kuwa idadi kubwa ya vijana walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 24 wanatafuta usaidizi kutokana na maswala tata ambayo hayajawahi kuonekana miongoni mwa wagonjwa walio na umri mdogo katika kipindi cha miaka 10.
Awali watu wazima ndio waliokuwa wakitembelea vituo vya afya wakikabiliwa na matatizo kama kushindwa kusimamisha uume kutokana na magonjwa kama vile sukari ama yale ya moyo.
Lakini utazamaji wa picha za ngono mitandaoni unaharibu mahusiano ya ndoa kwa kuwa vijana wengi wanavutiwa zaidi na picha za ngono katika mitandao badala ya binaadamu.