Aliyekuwa makamu wa rais wa Sudan Kusini Dkt Riek Machar, ameondoka nchini humo wiki chache baada ya mapigano makali kuzuka kati ya vikosi vyake na wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir mjini Juba.

Msemaji wake James Gatdet Diak alisema kiongozi huyo amefanikiwa kuhamia taifa jirani, ambalo hakulitaja jina.
Rais Kiir alimfuta kazi Dkt Machar mwezi uliopita.
Bw Taban Deng Gai aliteuliwa kuchukua nafasi yake.
Dkt Machar alikuwa awali amesema hatarejea Juba hadi kuwepo na kikosi cha wanajeshi wasioegemea upande wowote cha kumlinda.