Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Aug 22, 2016

Rio2016: Mkenya Eliud Kipchoge ashinda mbio za marathon

Mkenya Eliud Kipchoge aliwaacha wenzake wakimfuata nyuma kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kushinda medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanaume katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.
Kipchoge mwenye umri wa miaka 31 ambaye alishinda mbio za London Marathon mnamo mwezi Aprili alitawala mbio hizo na kumaliza katika muda wa saa mbili,dakika nane na sekunde 44.
Feyisa Lilesa wa Ethiopia alimaliza wa pili akiwa nyuma ya Kipchoge kwa sekunde 70 ili kushinda fedha naye raia wa Marekani Galen Rupp akimaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba.
Ushindi huo sasa unaipatia kenya medali yake ya sita kabla ya kukamilika kwa michezo hiyo siku ya Jumapili.
Kenya pia ilijishindia medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanawake katika siku ya kwanza ya mashindano hayo ambapo Jemimah Sumgong aliibuka mshindi.
Jemimah Sumgong aliyeishindi kenya medali ya dhahabu upande wa akina dada
Image captionJemimah Sumgong aliyeishindi kenya medali ya dhahabu upande wa akina dada

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP