Shughuli ya kuhesabu kura katika uchaguzi ulio na ushindani mkali inaendelea nchini Zambia huku kukiwa na wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kwa matokeo hayo.
Mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema ameishtumu tume ya uchaguzi kwa kuchelewesha matokeo hayo kwa makusudi .

Kwa upande wake tume hiyo ya uchaguzi imelaumu kuchelewa kwa matokeo hayo kutokana na idadi kubwa ya wapiga kura iliojitokeza ikiongezea kuwa inatarajia kutangaza matokeo hayo baadaye siku ya Jumapili.
Rais aliye mamlakani Edgar Lungu ,kwa sasa anafurahia uongozi mdogo dhidi ya Hichilema.