Urusi Imejibu kwa kauli nzito maamuzi ya mahakama moja ya kupiga marufuku ushiriki wa wanamichezo walemavu kutoka nchini Urusi , sababu kubwa ikitajwa kuwa ni utumizi wa dawa za kusisimua misuli na masharti waliyoyaweka na wadhamini.
Waziri mkuu wa Urusi,Dmitry Medvedev, amesema kwamba uamuzi huo ni wa kijinga na kwamba ni pigo kwa watu wote wenye ulemavu.

Wanamichezo walemavu kutoka Urusi nao wametoa kauli nzito kufuatia madai hayoImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionWanamichezo walemavu kutoka Urusi nao wametoa kauli nzito kufuatia madai hayo

Hata hivyo ametupilia mbali uchunguzi wa hoja ya dawa za kulevya kwa Urusi na kudai kwamba ni sawa na usaha,na ndani yake kuna msukumo wa kisiasa na mchanyato wa machukizo kwa wakati mmoja.
Wanamichezo walemavu kutoka Urusi nao wametoa kauli nzito kufuatia madai hayo na mmoja wao kuuelezea uamuzi huo kama wa kufedhehesha.