Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Aug 20, 2016

Usain Bolt ashinda dhahabu yake ya tatu Rio

Mwanariadha wa kasi zaidi duniani mzaliwa na Jamaica Usain Bolt amepata dhahabu katika mbio tatu tofauti katike kile kinachojulikana katika kiingereza kama "trible trible" au tatu tatu.

Shindano lake la mwisho lilikuwa la mita 100 kupokezana vijiti mara nne.
Alipokea kijiti mwisho katika timu yake na akafululiza kishujaa na kumshinda mpinzani wake wa karibu kutoka Japan, aliyeshinda Marekani na kuchukua Shaba.
Bolt ameshinda dhahabu mara tatu katika Olimpiki zote tatu alizoshiriki ndipo ushindi wake huu ukatambuliwa kama trible trible yaani tatu tatu.
Bolt mwenye umri wa miaka 29, alishinda dhahabu katika mbio za mita 100 na 200 mjini Rio na ndiye mwanariadha wa kwanza kushinda mbio tatu katika mashindano matatu ya olimpiki
Awali timu ya marekani ya wanawake ilishinda mbio sawa na hizo za kupokezana vijiti.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP