WADHAMINI WARUDISHA HADHI YA SHINDANO LA MISS TANGA 2016



 Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha 

akiwapungia mikono wananchi waliojitokeza kushuhudia shindano hilo mara 
baada ya kutangazwa kuwa mshindi



 Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha 

akiwapungia mikono watazamaji waliojitokeza akiwa na mshindi wa pili na 
tatu katika Shindano hilo ambalo liliandaliwa na Radio Tanga Kunani (TK)
na Hotel ya Tanga Beach Resort.


Warembo walioingia tano bora wakiwa jukwaani


Kamati
ya Miss Tanzania nao walikuwepo wakifuatilia shindano hilo ambalo
lilifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort mjini Tanga.


 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akizungu mza wakati wa shindano hilo

Msanii
Nevy Kenzo akitumbuiza wakati wa shindano la kumtafuta mlimbwende wa
mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)lililofanyika hivi karibuni kwenye hotel
ya Tanga Beach Resort
WAKATI shindano la kumsaka malkia
wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)likifanyika mwishoni mwa wiki na
hatimaye mrembo Eligiva Mwasha kuibuka na ushindi kwenye kinyang’anyiro
hicho dhidi ya washiriki wengine 10.



Shindano hilo ambalo lilisimama kwa muda baada ya serikali

kulisimamisha lile la Taifa msimu huu lilionekana kuwa na msisimuko wa
hali ya juu kuanzia wapenzi,wadau na washiriki iliyochangiwa na waratibu
wa shindano hilo Radio ya Tanga Kunani FM (TK) wakishirikiana na Hotel
ya Tanga Beach Resort.



Ushindani wa washiriki hao ulianza kuonekana tokea wakati warembo hao
wakiwa kwenye kambi yao ambayo ilifanyika kwenye hotel hiyo ambapo kila
mmoja alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuondoka na taji hilo.



Hali iliendelea kuwa ya mvutano zaidi baada ya baadhi ya washiriki

kuaga mashindano hayo na kutoa fursa yaw engine kuingia nafasi ya tano
bora katika kinyanganyiro hicho ambacho kilihudhuriwa na wapenzi wengi
kuliko kawaida.



Kitendo hicho kinaonekana kinawezesha kurudisha hamasa na heshima ya
shindano hilo ambalo hufanyika kila mwaka mkoani hapa lakini pia
kuhamasisha hasa vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki msimu ujao.



Katika shindano hilo nafasi ya pili ilichukuliwa na Aisha Ally huku

nafasi ya tatu ikitwaliwa na Rukaiya Hassani katika shindano hilo

ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kusheheni warembo wakali.



Halikadhalika nafasi ya mrembo kwenye kipaji katika shindano hilo

ilinyakuliwa na Edna Chisabo ambapo kinyang’anyiro hicho kilifanyika
siku moja kabla ya onyesho la kumsaka mrembo wa mkoa huu  kwenye ukumbi
wa Tanga City Lounge uliopo mjini hapa.



Licha ya kufanyika shindano hilo lakini yapo mambo ambayo kimsingi
yameweza kuleta msisimuko na kulifanya kuonekana kuwa na ubora wa hali
ya juu.



Mambo hayo ndio yamechangia kwa asilimia kubwa kupelekea shindano hilo
kuwa na mvuto mkubwa kuliko mashindano mengine ambaye yalikwisha
kufanyika mkoani hapa lakini pia uwepo wa  watazamaji wengi.



La kwanza ni eneo ambapo onyesho hilo limefanyika,moja kati ya mambo
ambayo yalichangia kuonekana kuwa na mvuta mkubwa ilitokana na shindano
hilo msimu huu kufanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort.



Tunasema hivyo kwa sababu kila mtu anapokwenda kuangalia burudani ya
aina yoyote lazima aangalia ulinzi na uimara wa eneo husika hasa
ukizingatia wapo baadhi yao huenda na vyombo vyao vya usafiri.



Kama ujuavyo ulinzi wa mahali husika ndio huwafanya watu kwenda kupata
burudani lakini pia ni eneo tulivu ambalowatu wanaweza kufanya mambo yao
kila kupata usumbufu wa aina yoyote.



Jambo hilo limesababisha baadhi wa watu kuacha kwenda kwenye maeneo
yaliyopo karibu nao na kwenda maeneo mengine ya mbali kwa ajili yakusaka
utulivu lakini pia ulinzi.



Jambo jingine ambalo lilisababisha onyesho hilo kuwa bora ni uwepo wa
warembo makini na wenye muonekana bomba na hivyo kupelekea wapenzi na
wadau wao kujitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange huo ambao ulikuwa wa
aina yake.



Kilicholifanya shindano hilo kuendelea kuvutia wapenzi na mashabiki
ambao walijitokeza  ni wasanii ambao walikuwa wakitumbuiza kabla ya
kuanza.



Wasanii wanaounda kundi la Nevy Kenzo wazee wa Kamati Chini ilikuwa ni
kichocheo kikubwa cha umati mkubwa wa wadau wa tasnia ya urembo na
burudani kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano .



Nevy Kenzo ambao walipanda jukwaani kutumbuiza walisababisha ukumbi
mzima kulipuka kwa shangwe na nderemo huku baadhi yao wakiimba nyimbo
zao ikionyesha namna wanavyokubalika.



Nevy Kenzo wakati akiimba ilifikia wakati mpaka wapenzi na mashabiki wa
tasnia ya urembo waliviona viti vyao vya moto na kulazimika kupanda
jukwaani kucheza sambamba na wasanii hao.



Haikuishia hapo lakini wasanii ambao walipanda jukwaani kabla ya Nevy
Kenzo kutumbuiza wa Kundi la Wazenji Classic lenye makazi yake mjini
Tanga walikuwa na moto na kusababisha shangwe  kila mahali.



Shangwe hizo zinaonyesha namna kundi hilo lilivyoweza kujizolea

umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanga hasa kwa kipindi kifupi kutokana
na aina ya mziki ambao wanaufanya staili ya mduara na bongo fleva.



Sababu kubwa ya kuona kundi hilo kuonekana litakuwa hatari ni namna
wanayoweza kulitawala jukwaa wanapokuwa stejini na kuonekana kuinua mara
kwa mara wapenzi na mashabiki wao



Suala jingine ambalo lilikuwa kivutio kikubwa ni namna warembo

walivyokuwa wakipanda jukwaani na kuanza kujitambulisha na kujielezea kwa watazamaji.



Hali hiyo ilisababisha wakati mwengine baadhi ya warembo kupanda
jukwaani kwa madoido makubwa kwa lengo la kuonyesha umahiri wao ili
kuwashawisha majaji kuwapa alama nzuri.



Mbunge wa Jimbo la Tanga atinga Miss Tanga.
 
Kitendo cha Mbunge wa Jimbo la
Tanga (CUF)Mussa Mbaruku kuhudhuria shindano la kumsaka mlimbwende wa
mkoa wa Tanga mwaka huu kilionyesha namna alivyokuwa kiongozi mpenda
michezo na kuithamini.




Mbunge huyo ambaye alikuwa kwenye shughuli zake za kikazi lakini
alilazimika kuungana na wakazi wa jimbo lake kumshuhudia mrembo ambaye
anapatikana.




Akizungumza mara kabla ya kutangaza mshindi wa Taji la Miss Tanga
2016,Mbunge Mussa alisema tasnia ya urembo imekuwa ikiwapa vijana maisha
mazuri lakini pia imekuwa ni daraja la wao kupata mafanikio




Alisema lazima watanzania ikiwemo wazazi kubadilika na kuondokana na
dhana ya kuwa  ya kuwa urembo ni suala la uhuni kwani imekuwa ikisaidia
vijana wengi kupata maendeleo.




  "Ndugu zangu lazima tubadilike na kuishi kutokana na utandawazi


uliopo ile dhana ya kuwa urembo ni uhuni mimi nadhani imepitwa na wakati
na uhuni mtu anaweza kuwa nao hata asiposhiriki mashindano hayo hivyo
wazazi na walezi ruhusuni watoto wenu washiri kwenye mashindano haya
"Alisema.




Mussa alisema kuwa anaamini washindi wa shindano hilo wataweza


kuuwakilisha vema mkoa wa Tanga kwenye mashindano ya Kitaifa na kuweza kushinda kama walivyofanya kwenye onyesho hilo.




  “Ninaimani kubwa na washindi ambao wamepatikana kwenye shindano hilo
wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko kwenye tasnia ya urembo mkoa huu
kwani wanaweza hata kuleta taji la Miss Tanzania msimu huu “Alisema.




"Neno la Mshindi wa taji la Miss Tanga 2016 Eligiva Mwasha" Alisema kuwa
kwanza anawashukuru wakazi wa Mkoa wa Tanga  kwa ujumla kwa sapoti yao
walionyesha katika  fainali za miss tanga 2016 na yeye kupata fursa ya 
kunyakua taji hilo




Licha ya kuibuka na ushindi lakini niwaombe niombea kwani kwa sasa
safari aliokua nayo bado kubwa sana kwani anamtihani  wakwenda
kuiwakilisha Tanga katika fainali za Miss Kanda  na  badae kulekea
Katika fainali za miss Tanzania baadae mwaka huu.