Wahamiaji 21 waliozama wameripotiwa kuzikwa na wakazi wa mji wa Libya baada ya miili yao kukutwa ikielea ufukweni.
Mamlaka nchini humo zinasema zililazimika kuchukua hatua ya kuondoa maiti zilizokuwa zinazagaa.

Bahari ya Mediterranea inayotumika na wahamiaji kwenda ng'ambo
Image captionBahari ya Mediterranea inayotumika na wahamiaji kwenda ng'ambo

Miili hiyo ilikaa siku tatu katika pwani ya Al- Maya, kaskazini mwa Tripoli .

Mohammed Garbaj amekuwa akijaribu kuwaokoa wahamiaji wanaozama
Image captionMohammed Garbaj amekuwa akijaribu kuwaokoa wahamiaji wanaozama

Wenyeji wa eneo hilo walijawa na hofu ya maiti hizo kusababisha magonjwa ndipo wakalazimika kuzizika.