Jana tarehe 23.9.2016 imeingia rekodi mpya kisiwani Zanzibar baada ya Ndugu Abdulhalim Mohamed kutokea Ubelgiji kupiga goti na kuhalalishiwa rasmi mkewe Mariam Abbas kisiwani Zanzibar.Pichani ni bwana harusi akiwa na mkewe Mrs Mariam Abdulhalim,waliosimama pembeni mwa maharusi ni rafiki wa karibu wa bwana harusi nao pia wote wametokea Ubelgiji kwa ajili ya sherehe hiyo

Mr & Mrs Abdulhalim..Wallah walipendeza sana

Bwana harusi Abdulhalim akiwa na wazazi wake upande wake wa kulia mwenye kanzu ya kijivu ni baba wa bwana harusi Mzee Said Salim ambaye ni mkazi wa United Kingdom [UK] na mama yake bi Salma Mbeto Khamis,na kwa upande wa kushoto mwa bwana harusi mwenye koti la rangi ya maziwa ni baba mkwe wa bwana harusi,Mzee Juma Muhunz..Ndoa ilifungwa kwenye msikiti wa Mombasa Unguja

Bwana harusi akipata picha ya pamoja na familia yake,kulia kwa bwana harusi ni wazazi wa bwana harusi na kwa upande wa kushoto waliovalia sare ni dada wa bwana harusi ambao ni Jamillah Said Salum na Zuhra Said Salum

Bwana harusi bwana Abdulhalim muda mfupi baada ya ndoa akipata picha na ndugu na marafiki zake wa karibu.

Bwana harusi akiwa na rafiki zake

Bwana harusi akipata picha ya pamoja na wazee wake waliohudhuria tukio la ndoa hapo jana

Bwana Abdulhalim jana ilikuwa siku yake maalumu katika historia ya maisha yake,hapo akipata picha na mzazi wake na baba mkwe wake

Maharusi wetu kwa siku ya jana kiukweli walipendeza sana,Pichani Mr Abdulhalim akiwa na mkewe Mrs Mariam Abdulhalim ndani ya ukumbi wa SHAA TIMBER uliopo Mombasa kisiwai Unguja tayari kabisa wakisubiri matukio muhimu kwa ajili ya shughuli yao.Allah awafanyie wepesi inshallah

Maharusi wakiingia holini SHAA TIMBER

Matukio ya picha yakiendelea kwa maharusi wetu

Mara baada ya ndoa kufungwa salama msikiti wa NIKAH,hapa ni nyumbani kwa bi harusi kitongojini Kisauni.Bwana harusi katika sura ya upole na unyenyekevu ukweni...

Mr na Mrs Abdulhalim wakipozi

Maharusi wakipata picha na wazazi wao


Baada ya ndoa kufungwa salama msikiti wa NIKAHA,bwana harusi akipewa mkono wa pongezi kwa hatua na sunna muhimu aliyoifanya hapoa jana..Ama hakika Abdulhalim unastahili pongezi

Uuungwana ni vitendo,kitendo alichokifanya kijana Abdulhalim  kinastahili pongezi na hapo ndipo picha inadhihirisha kinachostahili

Ni sunna kumshika kichwa mkeo na kuomba dua juu ya ndoa yenu,Pichani bwana Abdulhalim akifanya kile kinachostahili kwa mkewe.Allah barik ndoa yao inshallah.



Kioo hakindanganyi bi harusi alipodolewa kapodoka mashallah..Uongozi mzima wa Maganga One Blog unwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape kila la heri na baraka kwenye ndoa yenu,na mkijaaliwa watoto inshallah wawe watoto wa heri.