Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Sep 27, 2016

Uchaguzi wa wabunge Somalia waahirishwa

Mchakato wa kuchagua bunge jipya nchini Somalia umeahirishwa.
Takriban wajumbe 14,000 walistahili kuchagua bunge la juu na la chini mwishoni mwa wiki lakini hata hivyo hakuna kura iliyopigwa.
Hatua hiyo itaathiri uchaguzi wa Urais

Hakuna sababu iliyotolewa, lakini ripoti kutoka nchini Somalia zinasema kuwa kuna tofauti ambazo hazijatatuliwa kuhusu ni vipi mchakato huo utakavyoendeshwa.
Mipango ya watu kupiga kura ilitupiliwa mbali kutokana na ukosefu wa usalama na miundo msingi.
Mabunge hayo mawili yanastahili kumchagua rais ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao.
Vilvile uchaguzi wa urais utafanyika mwezi Novemba tarehe 30.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP