Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Sep 29, 2016

Zaidi ya 100 wajeruhiwa kwenye ajali ya treni Marekani

Treni moja imegonga kituo cha reli kwenye mji wa Hoboken ulio jimbo la New Jersey nchini Marekani
Idara inayohusika na huduma za dharura jimba la New Jersey inaripoti kuwa watu watatu wameuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa .

Picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha uharibifu mkubwa kwa treni na kituo.

Kituo cha Hoboken kiko umbali ya maili ksaba kutoka mji wa New York
Image captionKituo cha Hoboken kiko umbali ya maili ksaba kutoka mji wa New York

Kituo cha Hoboken kiko umbali ya maili saba kutoka mji wa New York na watu wengi hukitumia kusafiri kwenda mtaa wa Manhattan.
Ben Fairclough ambaye alikuwa eneo hilo aliiambia BBC kuwa treni hiyo ilikuwa imetoka kabisa kwenye njia yake.
"Kulikuwa na watu waliokuwa wameketi chini huku damu ikiwatoka vichwani. Kulikuwa na majeruhi wengi," alisema Fairclough.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP