Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Sep 24, 2016

Zari, Mobeto Kimenuka Tena!

 
Mwanamitindo Hamisa Mobeto.
DAR ES SALAAM: Kimenuka tena! Ndiyo unavyoweza kusema baada ya mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutupia picha ya hereni kwenye Mtandao wa Kijamii wa Snapchat huku akitupa dongo kwa kusema aliyesahau vitu vyake aende akavitoe, bifu limeibuka upya mitandaoni.
 
zari
Mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Baada ya kutupia picha ya Snapchat hiyo, mashabiki mbalimbali wa mtandao huo walijiongeza na kuoanisha na picha ya Mwanamitindo Hamisa Mobeto kwa kufananisha hereni alizovaa siku za nyuma zikifanana na hizo alizodai Zari zimesahaulika kwenye chumba cha Diamond, nyumbani kwake, Tegeta-Madale jijini Dar.
Mbali na mashabiki hao kujiongeza, mjadala mzito uliibuka pia wakidai ugomvi wa Zari na Mobeto si rahisi kumalizika maana kati yao hakuna anayeweza kuwa mpole na kumwachia mwenzake atambe. “Hili lazima ni dongo kwa Mobeto, yaani hawa, hauwezi kupita muda hawajazinguana, kweli mapenzi yanauma lol…” aliandika mmoja wa mashabiki wanaotumia mtandao huo wa Snapchat.
     Staa wa Bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake Zari .
Mjadala ulikuwa mkubwa huku kila mmoja akimtetea anayempenda hadi mashabiki hao kufi kia hatua ya kutukanana mitandaoni. Kuna ambao walimtetea Zari lakini wengine walikuwa upande wa Mobeto.
Risasi Jumamosi lilimtafuta mwanamitindo huyo ili aweze kufungukia hayo madai ambapo alisema ameziona lakini hakutaka kufunguka kama ni zake au la: “Nimechukizwa na kitendo hicho. Kitendo hicho kimenifanya mimi nitukanywe sana matusi ya nguoni kwenye mitandao ananitafuta sana Zari lakini ipo siku atanipata,” alisema Mobeto. Hii si mara ya kwanza kwa wawili hao kuingia kwenye bifu ambapo inadaiwa penzi la Diamond ndilo linalowatia ‘uchizi’ hata kuwafanya w a k w a r u z a n e k i l a mara
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP