Mkurugenzi wa TEA Joel
Laurent katikati akiangalia darasa la Tehama Computer ambazo baadhi zilitolewa
kama msaada na TEA kwa shule hiyo.

na fredy mgunda,Iringa. 

MBUNGE wa jimbo la mafinga
mjini cosato chumi amewataka wananchi kuendelea kujituma kufanya kazi wakati
akitafuta ufumbumzi wa kero na changamoto mbalimbali za jimbo hilo jimpya.


Aliyasema hayo alipokutana
na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bw Joel Laurent katika Shule ya
makalala yenye mahitaji maalumu huku lengo likiwa ni kumuonyesha mkurugenzi
huyo jinsi hali ilivyombaya ya kitaalum na mazingira yalivyo magumu kwa
wanafunzi wenye mahitaji maalumu.


“Ninajitahidi kufanya kila
kinachowezekana ili mradi kutatua changamoto za wananchi wa jimbo la mafinga na
kuleta maendeleo kadili ninavyoweza” alisema chumi 


 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Elim Tanzania Bw Joel Laurent alisema kuwa atatuma timu yake ya wataalam kwa
ajili ya kufanya tathimini ya mahitaji ya miundombinu katika Shule ya Msingi
Mchanganyiko ya Makalala iliyopo Mafinga.


Bw Laurent aliyasema hayo siku
Alhamis alipoitembelea Shule hiyo kufuatia ombi la Mbunge wa Mafinga Mjini.


Mkurugenzi huyo alisema
kwamba TEA pamoja na mambo mengine Ina wajibu wa kusaidia miundombinu na vifaa
saidizi vya kufundishia na kujifunzia na kwamba Mwaka huu wataelekeza nguvu
katika Shule za mahitaji maalum kama Makalala na kwa wanafunzi wenye mahitaji
maalum katika Shule za kawaida.


Shule hiyo yenye uwezo wa
kuhudumia wanafunzi 48 wa bweni wenye ulemavu wa akili, wenye ualbno na wenye
uono hafifu inakaribiwa na uhaba wa Bweni ambapo kwa Sasa wanafunzi
wanalazimika kulala mpaka watoto Sita katika baadhi ya vyumba.




Naye mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamu alisema kuwa anaishukuru TEA kwa kuitikia wito wa kuitembele shule hiyo yenye mahitaji maalumu na kuomba serikali kuwapa ushirikiano kutatua changamoto za shule ya makalala sambamba na kuwaomba wada wengine kuendelea kuisadia shule hiyo.



Wiki  iliyopita TEA ilitoa msaada wa vifaa visaidizi vya kusomea katika shule ya Ilboru sambamba na kukabidhi fimbo nyeupe mkoani Mbeya.