Marekani na Urusi wanafanya jitihada upya za kuendelea na mazungumzo yao juu ya kusitisha mapigano nchini Syria.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov na mwenzake wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry watakutana siku ya jumamosi huko Uswizi kwa ajili ya mazungumzo, nchi nyingine zitakazohudhuria mazungumzo hayo ni Saud Arabia, Turkey na Iran.

Lavrov amesema kuwa ana matumaini juu mazungumzo hayo.
Washington walivunja makubalioano yote na Moscow wiki iliyoita kufuatia kushindwa kwa usitishwaji wa mapigano nchini Syria.
mashambulizi yanaendelea eneo linaloshikiliwa na waasi mashariki mwa mji wa Aleppo.
Waokoaji wanasema kuwa angalau watu 25 wameuawa siku ya jumatano. mazungumzo hayo yanakuja baada ya siku mbili za mashambulizi mapya ya ndege huko Aleppo.