Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Oct 11, 2016

Mauaji ya Habyarimana: Rwanda yaionya Ufaransa

Rais wa Rwanda ,Paul Kagame ameonya kuhusu makabiliano na Ufaransa kufuatia tangazo la wachunguzi wa Ufaransa kwamba watafungua upya uchunguzi kuhusu mauaji ya aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana.

Kutunguliwa kwa ndege yake iliokuwa na wafanyikazi wa Ufaransa mwaka 1994 ilizua mauaji ya kimbari ambapo mamia ya maelfu waliuawa ,hususan watu wa kabila la Tutsi .
Uchunguzi huo umeanzishwa upya ili kupata ushahidi kutoka kwa jenerali aliyetoroka Rwanda Faustin Kayumba Nyamwasa ambaye anasema kuwa rais Kagame alihusika .
Mwaka 2006,Rwanda ilikata uhusiano wake na Ufaransa kwa miaka mitatu baada ya jaji kumtaka rais Kagame kujibu mashtaka.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP