Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya katika shambulio lililotokea Kaskazini mashariki mwa Mali.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani katika eneo hilo -MINUSMA- kimesema majeruhi walikuwa katika magari mawili yaliyoshambuliwa vibaya na mlipuko.

Kikosi hicho cha jeshi kilikuwa kikitafuta chanzo cha kombora lililo shambulia kambi yao siku ya Jumatatu.
Kikosi hicho cha jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Mali kimekuwa kikikabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na wapiganaji wa kiislamu na wale wa kikabila tangu kilipotawanywa nchini humo miaka mitatu iliyopita.