Ripoti kutoka eneo la kati la Ethiopia, zinasema kuwa kumetokea ghasia nyengine baina ya askari wa usalama na waandamanaji wanaopinga serikali, na watu kadha wamekufa katika mkanyagano.
Shirika la habari la Reuters, limewanukuu walioshuhudia tukio hilo, wakisema kuwa polisi walifyatua risasi na moshi wa kutoa machozi, wakati wa sherehe katika mji wa Bishoftu, jimbo la Oromiya.

Haijulikani kama kuna maafa yoyote yaliyotokea.
Eneo hilo pamoja na jimbo jirani la Amhara, yamekuwa na mapambano kwa miezi kadhaa na mamia ya watu wameuwawa huku watu wa huko wanazidi kuandamana kupinga kile wanachosema, ukandamizaji unaozidi kufanywa na serikali.
Wakuu wanasema maandamano hayo yanachochewa kutoka nchi za nje.