Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea  bajeti mbalimbali  za
waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo(picha na woinde Shizza wa libeneke la kaskazini


Arusha)






Nabii
mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiwa anahubiri katika
hema
la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha hii
leo
 Nabii mkuu akiwa anaendelea na huduma
ya sikuu kuu ya kukusanya hii leo




Nabii akiwa anamwaga upako kwa waumi
waliouthuria katika siku kuuu hii ya kukusanya hii leo (picha na
Woinde Shizza,Arusha )










 Nabii
mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea  bajeti mbalimbali  za
waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii
leo 








 Habari picha na woinde
shizza,Arusha
Watumishi  wa madhehebu
mbalimbali hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kuwasaidia yatima ili nao
waweze kujisikia kama wao ni sehemu ya jamii







Hayo yamebainishwa leo na Nabii mkuu
mheshimiwa Dr Geordavie
wakati akifanya  dua maalumu ya kupitisha
bajeti ya watu walioshiriki katika sikukuu ya kukusanya iliyofanyika katika
hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini
Arusha.







Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtumishi
kukusanya  na kutoa kile alichonauwezo nacho
ili  kuweza kuwasaidia watoto yatima ,wananchi
wasiojiweza  ili kuweza kuwafanya nao
wajisikie ni sehemu ya jamii







Alisema kuwa mbali na watoto yatima pia
aliwasihi makanisa
ambayo yanajiweza kuweza kusaidia yale ambayo ni machanga ili kuweza kuwapa
nguvu ya kuweza kuendelea kueneza injili na kumtangaza
mungu  kupitia makanisa yao
.



  Nabii
mkuu Dr Geordavie alisema kuwa  kuwa lengo la
sikukuu hii ya kukusanya
nikuwasaidia watoto yatima kwa kuwapa chakula kama mchele, sukari pamoja na
mafuta yakupikia ili nao wajisikie wanafuraha haswa katika kipindi hichi cha
sikukuu.



Alisema kuwa  licha ya
misaada hiyo kwenda kwa watoto yatima, pia atatoa fedha kwa watumishi wa mungu
wenye makanisa madogo hapa nchini lengo likiwa ni kuinua huduma zao na
kuwasaidia katika kuendeleza huduma zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kanisa,
ununuzi wa vyombo vya muziki na shughuli nyingine za
kanisa.



Sikukuu hii ya kukusanya
 huadhimishwa na huduma ya Ngurumo ya Upako
Duniani tarehe 26 ya kila mwaka, watu hutoa sadaka ya vitu mbalimbali ikiwemo
fedha kwa mujibu wa maelekezo ya Nabii Mkuu na kisha hugawanywa kwa vituo vya
watoto yatima  huku  fedha
zikigawanywa kwa watumishi waliotuma
maombi ya kupata msaada   wa kuendeleza
huduma zao.



Mwaka jana msaada wa zaidi ya shilingi
milioni 15 ulitolewa
na waumini wa kanisa la Ngurumo ya upako na kugawanywa katika vituo mbalimbali
vya watoto yatima huku fedha zikigawiwa kwa baadhi ya makanisa
madogo  kwa ajili ya kuwasaidia mambo mbalimbali
.