Mbunge wa
viti maalum mkoa waIringa(CCM) Rita Kabati akiongea na familia
ya watu watano wenye
ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi
kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wakati wa kuwasaidia msaada kukarabati nyumba yao pamoja na kuwapa vitu vingine vya kimsaada

Leah mwamoto mtoto wa mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto naye alishuhudia maisha magumu wanaoishi familia ya watu watano wenye
ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi
kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa na hapo aliposimama ndio choo kinachotumiwa na familia hiyo kwa sasa huku wakisubili ujenzi wa choo kipya kinachoendelea kujengwa kwa hisani ya mbunge Ritta kabati
 Hivi ni baadhi ya vifaa vilivyoletwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama
cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati kwa ajili ya kuwasidia
familia ya watu watano wenye
ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi
kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa

Na fredy mgunda,Iringa

FAMILIA ya watu watano wenye
ulemavu wa viungo wamemuomba mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama
cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati kuendelea kuilea familia hiyo kama familia
yake.

Akizungumza na blog hii
mmoja wa wanafamilia
hiyo,Elias Mpogole ambaye ni mlemavu alisema kuwa
mbunge huyo amekuwa akiwasaidia toka siku ya kwanza walipokutana naye katika
kijiji hicho cha Lulanzi.

“Zamani tulikuwa tunaishi
kwenye nyumba ambayo inavuja haina dilisha wala mlango pia tulikuwa tunalala
chini lakini mbunge Kabati katusaidia nyumba nzuri kama mnavyoiona waandishi,katuletea
magodoro,mashuka,blanket na sasa ameanza kutujenga choo cha kisasa na
ameshawalipa mafundi pesa zote ndio maana tunaomba anendelee kuwa na sisi.”Alisema
Mpogole

Mpogole alishukuru msaada
waliopatiwa na kuwataka wadau wengine waweze kujitokeza zaidi kuwasaidia
kuwapatia vyakula na radio za kuwezakusikiliza nyimbo za dini.

Kwa upenda wake mbunge wa
viti maalum mkoa waIringa(CCM) Rita Kabati ametoa msaada wa vitu mbalimbali
ikiwemo ukarabati wanyumba kwa familia yenye watoto walemavu wanne wa kijiji
cha Lulanzi kilichoko kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa. 

Msaada huo wa ukarabati wa
nyumba,umeambatana na magodoro, vyakula na ujenzi wa choo cha kisasa ameutoa
baada yakuwahidi kufanyia matengenezo ya nyumba ambayo walikuwa wakipata shida
kipindicha masika mara baada ya kufanya ziara mapema mwaka huu katika kijiji
hicho nakugundua mateso wanayokumbana nayo familia hiyo. 

 "Nimeitembelea familia hiinimeumia sana
kwani maisha wanayoishi ni ya shida sana hawana msaada wowotenyumba yao inavuja
hawana chakula maishayao ni ya kuunganga unga mpaka watu  wajekama sisi kuwaletea vitu  vidogo vidogokama mchele na mafuta na mbaya Zaidi
hata watoto hao wote watatu hakuna hatammoja aliyewahi kukanyaga shule ingawa
wanaonekana ni wakubwa hivyo jamii tunapaswa kuwasaidia watoto hawa” alisema Kabati  

Familia hiyo ambayo baba
mzazi Mzee LucasMpogole mbaye kwa sasa amelazwa hospitali ya mkoa wa Iringa kwa
ugonjwa wakupooza ina watoto wanne wote wakiwa walemavu wa viungo hivyo kukosa
msaadakabisa pindi mvua zikianza kijiji hapo. 

Akizungumza wakati wa
kukabidhimsaada huo , Kabati alisema kuwa jamii ya walemavu wanahitaji msaada
wa hali namali kutoka kwa wadau wenye uwezo na kuacha tabia ya kuiacha serikali
peke yakekatika kutatua kero zao na kuwahudumia.

Alisema kuwa msaada huo
utawafarijiwalemavu hao waone kuwa pamoja na upungufu walionao bado jamii ya watanzaniainawathamini
na kuwajali katika maisha yao ya kila siku.

 Aliongeza kuwa walemavu wanayo hakiya kuishi
na kujitegemea iwapo jamii itawajengea uwezo badala ya kuwafungiandani na
kuwaona kama ni mkosi katika familia ila kugundua vipajiwalivyonavyo na
kuiwezesha serikali kuwaingiza katika mipango mbalimbali yakuwapatia huduma. 

Kabati alitoa wito kwa
serikalikuona umuhimu wa kutumia vituo mbalimbali vinavyolea watoto wenye ulemavukuhakikisha
vinawejengea miundo mbinu rafiki na uboreshaji mipango na mfumo wautoaji elimu,
afya na usafiri kulingana na tofauti za umri wa watoto nchini. Aidha Kabati alitoa
wito kwa Mfukowa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuangalia kwa jicho la tatu familia
ya Mpogolekwa kuwaongezea kipato zaidi cha kila mwezi kwani kwa hali waliyonayo
nakiwango wanachopata kila baada ya miezi miwili hakiendani na uwingi wa
walemavuwa familia hiyo maskini. 

Naye baba mdogo wa watoto hao
akiongea kwa niaba ya baba mzazi wa walemavu hao, Juma Mpogole alimshukurumbunge
huyo kwa msaada aliotoa na kumtaka awasomeshe watoto wake ambao tangu wazaliwe
hawajawahi pata elimu yoyote licha ya kufikisha umri wa miaka zaidi 20.

Lakini naomba nitoe rai kwa
wale wanasiasa na wananchi wengine wanaokuja kupiga picha nah ii familia ya
watu wenye ulemavu wa viungo kwa ajili ya kujitafutia umaarufu waache tabia
hiyo.

“Kila mara tunaona waandishi
na wapiga picha wanafika hapa na viongozi mbalimbali lakini kila siku wanatoa
ahadi tu sioni msaada wowote ule unaotolewa zaidi ya kuona wanajitafutia
umaarufu huko mitaani naomba waacha tabia hiyo sisi tunamuona mbunge Ritta
Kabati na kaka yake mbunge wa jimbo hili la kilolo Vennence mwamoto ndio
wanaosaidia familia hii,kweli familia hii inaitaji msaada hivyo njooni kutoa
msaada sio kupiga picha pekee yake”.alisema Mpogole