mkurugenzi miliki na miradi wa miradi wa kituo cha mikutano cha AICC
Victoria Kamagenge akiwa anawaonyesha kamati Ya uwekezaji wa mitaji ya
uma  PAC moja ya mradi unaojegwa na kituo cha mikutano cha AICC  jijini
Arusha mradi unaogarimu kiasi cha shilingi bilioni 2.8





 baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC) wakiwa wanateta jambo


 wakiendelea kukagua
 mbunge wa jimbo la  Bunda mjini   Ester Bulaya akiwa
anakula na wakandarasi wa jengo jipya la maonyesho linalojengwa na kituo
cha mikutano cha AICC wakati walipofanya ziara na
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC


Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC) wakiwa katika picha ya pamoja
Na Woinde Shizza,,Arusha




Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PAC)
imeyataka mashirika ya umma 265 yalilopo hapa nchini, kuanza kujiandaa
kuchangia bajeti ya  serikali kuanzia
mwaka ujao wa fedha .




Aidha wakurugenzi na wenyeviti wa bodi wa mashirika
hayo kuanzia mwakani  watatakiwa  kuwasilisha bajeti zao bungeni ili kuweza
kupitishwa na bunge na hakuna shirika lolote la serikali litakaloweza kupiitishwa  bajeti bila kuithinishwa  na bunge.




Hayo yamebainishwa na mwenyekiti  wa kamati hiyo  ,Albart Obama Mtabaliba mbunge wa jimbo la
Buhigwe, mkoani Kigoma, wakati kamati hiyo ilipotembelea miradi ya kituo cha
kimataifa cha mikutano (AICC)nakujionea miradi mbalimbali inayoendeshwa na
kituo hicho ikiwemo ujenzi wa nyumba za kupangisha ,hosp italpamoja na jengo la
maonyesho na mikutano linaloendelea kujengwa na kituo hicho.




Alisema kuwa  licha ya mashirika hayo kuwa na thamani kubwa ya
shilingi trilioni 26 lakini yamekuwa hayachangii ipasavyo bajeti ya serikali
,hivyo yanatakiwa  yabadilike na kuanza
kulipa kodi ipasavyo pamoja na kutoa gawio serikalini.




‘’Mashirika yote ya umma yaliyopo hapa nchini
yanadhamani ya shilingi trilioni 26 na kwa mwaka yamekuwa yakitoa faida ya
shilingi bilioni 450 pekee ,ambayo ni sawa na asilimia 1.08% kitu ambacho hakiwezekani
ukilinganisha na mtaji uliopo wa trilioni 26
,na hivyo wakurugenzi na wenyeviti wa bodi wametakiwa wahakikishe mapato
yao kwa serikali yanapanda na angalau weweze kuchangia trilioni mbili kwa mwaka
“alisema Mtabaliba




Akizunguzia kituo  cha mikutano cha kimataifa  AICC alipongeza miradi inayoendeshwa na kituo
hicho na kushauri  waanze kuchukuwa hatua
ya kuanza kukabiliana na soko na pia wajitahidi kuwekeza zaidi katika ujenzi wa
vituo vya mikutano vya kisasa ,na kuwataka kuelekeza nguvu zaidi ya kujenga
kituo kikubwa cha mikutano katika mji mkuu wa Tanzania  ambapo ni Dodoma.




Hata hivyo mmoja wa  wabunge wa  kamati hiyo,Ester Bulaya alikosoa  gharama za ukarabati zilizotumika kukarabati
ukumbi wa Simba hall  uliopo katika kituo
hicho ambapo kiasi cha shilingi bilioni tatu na nusu zilitumika jambo ambalo
hawakuafiki na kushauri kwamba fedha hizo ninyingi sana na zingeweza kutumika
kwenye uwekezaji mwingine .




Naye mkurugenzi mtendaji  wa AICC
Elishilia Kaaya  alisema kuwa
amefurahishwa  na ujio wa kamati hiyo
kuwatembelea  na pia wamekutana nao na
wamepewa elimu nzuri ya uwekezaji na wametaza baadhi ya  mambo yale ambayo ayajaenda sawa
wamewarekebisha pale ambapo awapo vyema wamewafundisha hivyo wanaamini  walivyoambiwa mtazamo ubadili utabadilika
kulingana na hali ilivyo.




Hata hivyo alisema kwa sasa wameanzisha mradi
ujenzi wa kumbi za mikutano,mahoteli na maonyesho  unaogarimu kiasi cha shilingi shilingi bilioni
2.8,mradi ambao unatarajiwa kukamilika mapema May 4 ambapo wanategemea
utasaidia kuongeza mapato ya kituo hicho pamoja na ajira kwa watanzania.