Crystal Palace imeendelea kurudisha matumaini ya kusalia kwenye ligi kuu ya England baada ya kuichapa Arsenal ambayo nayo inahaha kuingia nafasi ya nne baada ya kukumbana na wakati mgumu.

Iwapo Arsenal itashindwa kuingia nafasi nne bora, itakuwa ni mara ya kwanza tokea imeanza kunolewa na Arsene Wenger mwaka 1996.
Palace wameshinda kwa magoli 3-0 katika mchezo uliokuwa wa kusisimua.
Sam Allardyce hana rekodi ya kushusha timu daraja
Image captionSam Allardyce hana rekodi ya kushusha timu daraja
Palace walianza kuongoza kupitia kwa Andros Townsend kisha dakika chache baadaye Yohan Cabaye akapachika goli la pili.
Mashabiki wa Arsenal bado wanataka Wenger aondoke
Image captionMashabiki wa Arsenal bado wanataka Wenger aondoke
Luka Milivojevic akaiandikia Palace goli la tatu kwa mkwaju wa penalti na kuifanya kuwa alama sita juu ya mstari wa kushuka daraja.
Katika kipindi cha pili Arsenal hawakuweza kupiga shuti lililolenga lango la Palace.
Tokea ajiunge na Arsenal mwaka 1996, Wenger hajawahi kumaliza nje ya nne bora
Image captionTokea ajiunge na Arsenal mwaka 1996, Wenger hajawahi kumaliza nje ya nne bora
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal waliosafiri kutoka London walibeba mabango yanayomtaka mfaransa huyo kuachia ngazi.
Palace kwa sasa wamejikusanyia alama 34
Image captionPalace kwa sasa wamejikusanyia alama 34
Arsenal ipo alama saba nyuma ya timu ya nne ambayo ni Manchester City ikiwa pia imesalia na michezo nane kabla ya ligi kumalizika.