Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Apr 8, 2017

Bruno Tshibala ndiye waziri mkuu mpya DR Congo

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila, amemteua Bruno Tshibala kama Waziri Mkuu mpya katika Serikali ya kugawana madaraka.
Bwana Tshibala ataongoza taifa hilo hadi uchaguzi wa Urais unaotazamiwa kufanywa baadaye mwakani.

Alitimuliwa kutoka chama kikuu cha upinzani, UDPS, mwezi uliopita baada ya kupinga watu waliochaguliwa chamani kuchukua madaraka ya kiongozi aliyefariki Februari, Etienne Tshisekedi.
Waandishi wa habari wanasema kuwa kuchaguliwa kwa Bwana Tshibala kutawagawanya zaidi wapinzani wa Bwana Kabila baada ya mashauriano ya kujadili jinsi atakavyoondoka mamlakani kuporomoka juma lililopita.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP