'All Eyez On Me' ni filamu ya muigo wa maisha ya msanii huyo ikieleza hadithi ya alivyopanda ngazi hadi akawa mtu maarufu na hali tata iliyomzingira alipokuwa juu.
Pia itaangazia kifo chake ambacho kilitanda kote ulimwenguni.

Aliuza mamilioni ya rekodi dunia nzima, na siku ya Ijumaa akawa rapa wa sita kuingizwa kwa ''Rock and Roll Hall of Fame'' (wasanii waliovuma)
Demetrius Shipp Jr. ndiye atakayemuigiza Tupac katika filamu na ni mchezo wake wa kwanza mkubwa.
Msanii Tupac Shakur alifariki Septemba mwaka wa 1996 mjini Las Vegas baada ya kupigwa risasi mara nne.
Image captionMsanii Tupac Shakur alifariki Septemba mwaka wa 1996 mjini Las Vegas baada ya kupigwa risasi mara nne.
Danai Gurira, kutoka filamu ya the Walking Dead, pia atacheza kama mamake Tupac.
Kipande kifupi cha maelezo ya filamu hiyo kinaanza na maneno '' lazima uwe na msimamo wa kitu fulani, lazima uishi kwa sababu ya kitu fulani, na lazima uwe tayari kufa juu ya kitu fulani''
Inaonyesha Tupac akiwa katika studio ya kurekodi nyimbo na akiimba mbele ya watu, na dakika chache baadaye kunatokea vurugu la bunduki na kutajwa katika uchunguzi na idara ya upelelezi FBI.
Demetrius Shipp Jr. ameigiza kama Tupac Shakur.Haki miliki ya pichaCODEBLACK FILMS
Image captionDemetrius Shipp Jr. ameigiza kama Tupac Shakur.
Tupac Shakur alizaliwa jijini New York, lakini aliishi California.
Wakati wa umaarufu wake hakuwa anasikizana na wasanii wenzake wa rap kutoka pwani ya mashariki akiwemo P Diddy na Notorious B.I.G.
Bali na usanii wake pia alitokea kwa filamu kadhaa ikiwemo filamu ya magenge, na filamu ya mchezo wa vikapu, Above The Rim.
Alifariki Septemba mwaka wa 1996 mjini Las Vegas baada ya kupigwa risasi mara nne.
Alipelekwa hospitali lakini akaaga dunia siku sita baadaye akiwa na umri wa miaka 25.
Aliyemuua hajawahi kupatikana.
Filamu hiyo itatolewa tarehe 16 mwezi Juni