Matumaini ya Sunderland yamedidimia kwa mara nyingine baaada ya kutandikwa na Manchester United mabao 3-0.
Ushindi huo unaiwezesha Man U kupanda hadi nafasi ya tano katika jedwali.

Sunderland ilicheza na kikosi cha watu 10 baada ya Sebastian Larsson kupewa kadi nyekundi alipomchezea vibaya Ander Herrera.
Wakati huo Zlatan Ibrahimovic alikuwa taraia ameiweka Mancheter United kileleni kwa bao moja.
Henrikh Mkhitaryan aliifunga bao la pili huku naye Marcus Rashford akifunga bao la tatu.
Sunderland wanatafuta pointi 10 kujiokoa kutimuliwa kutoka ligi huku wakiwa na mechi 7 pekee za kucheza wakiwa hawajafunga goli katika mechi saba.
United, wamewapiku Arsenal wakiwa pointi nne nyuma ya Manchester City.
Manchester United waitandika Sunderland bao 3-0Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionManchester United waitandika Sunderland bao 3-0