Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athumani Juma Kihamia


Na Mwandishi Wetu, Arusha



Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athumani Juma Kihamia amefanya
kikao na watumishi wa serikali katika Kata ya Muriety na Terati na
kuzungumza mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha utendaji kazi
wao.




Kihamia amesema kuwa lengo hasa la kuonana na watumishi hao ni
muendelezo wa ziara yake ya kutembela kila Kata na kuwakumbusha
watumishi hao jinsi ya kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya
Raisi John Magufuli.



“”Siyo kwamba watumishi wangu wa Halmashauri hawafanyi kazi Bali ni
kuwakumbusha majukumu yao katika kutumikia wananchi hasa katika kasi ya
serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu ambayo inatutaka tuwe karibu
zaidi na wananchi wetu na Mimi kama Mtendaji mkuu lazima nisimamie
kikamilifu “” Alisema Mkurugenzi Kihamia



Vile vile amesema kuwa watendaji wa serikali wanatakiwa wajitume kwa
nguvu zote wasisubiri mpaka viongozi wa juu wafike kwenye maeneo yao na
wananchi walalmike wakati kuna kiongozi katika eneo hilo ambaye analipwa
na serikali ili kusaidia wananchi.



“” Hatutaki Mwananchi atoke kwenye Kata mpaka kwa mkuu wa Mkoa au
mkuu wa Wilaya wakati kwenda kumlalamikia masuala madogo madogo wakati
kuna kiongozi ambaye tumemuweka ili atatue kero akitokea Mtumishi wa
hivyo ajue kwamba hatoshi kuongoza wananchi “”Alisema Kihamia



Ameongeza kuwa kwasasa anahakikisha Huduma zinaboreshwa katika jiji
la Arusha kwa kumjengea Mtumishi uzoefu wa kufanya kazi bila kuogopa
changamoto zilizopo na kuwa jasiri wakati anaongoza wananchi kwenye
maeneo yao.



Hata hivyo amewagiza watumishi hao wa serikali wakiwemo watendaji
kutekeleza kwa muda uliowekwa mambo muhimu kama vikundi vya vijana na
Wanawake, kuainisha maeneo ya biashara na idadi yake ikiwemo mabango Na
maduka yote,majengo na miradi viporo pamoja na kuainisha Yale maeneo
yote ya wazi.