Rais wa Iran Hassan Ruhani mesema kuwa ''magaidi'' wanasherehekea shambulio la Marekani katika kambi moja ya jeshi ya Syria.
Matamshi yake yanaunga mkono yale ya Urusi ambayo kama Iran inaunga mkono Syria.

Takriban watu sita wameripotiwa kufariki katika shambulio hilo mapema siku ya Ijumaa.
Mashambulio hayo yanajiri kufuatia madai ya shambulio la kemikali ya sumu katika eneo linalomilikiwa na waasi mjini Khan Sheikhoun ambapo takriban watu 89 walifariki.
Syria imekana kutumia gesi ya nevi na badala yake imesema wanajeshi wake walishambulio kituo kimoja ambapo waasi wanahifadhi silaha za kemikali ya sumu.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza Boris Johnson amesitisha ziara yake mjini Moscow akisema hali imebadilika na kwamba atashirikiana na Marekani kutafuta mwafaka wa usitishwaji wa vita.
Katika mji wa Damascus na dunia nzima, watu walipinga mshambulio hayo ya Marekani wakisisitiza kuwa Marekani haifai kuwa na vita dhidi ya Syria.