Rais wa Marekani, Donald Trump ametia saini amri ya kupitia upya mpango wa Visa zinazotumika kuwaruhusu wageni kufanya kazi maalum nchini Marekani.
Amri hii inayataka mashirika kufuata taratibu za Serikali katika kuondoa wafanyakazi wa kigeni kwenye mpango wa kuwania zabuni kwenye miradi ya serikali.

Trump ametia saini amri aliyoiita ''Nunua bidhaa za Marekani, Ajiri wamarekani'' alipofanya ziara kwenye kiwanda kimoja katika jimbo la Wisconsin
Amri hii ina nia ya kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa Kampeni ya ''Marekani kwanza''.
Trump atatoa maelekezo kwa idara ya mambo ya ndani, sheria, usalama wa ndani na kazi na kupendekeza kufanyia mabadiliko mpango huo, ambao unawaruhusu waajiri wa nchini humo kuwapa wageni nafasi za kazi.
''kwa hatua hii tunatuma ujumbe wenye nguvu kwa dunia kuwa tutatetea wafanyakazi wetu, kulinda kazi zetu na pia kuiweka Marekani mbele''.
Mke wa Rais Donald Trump, Melania alitumia Visa ya muda iliyompa nafasi ya kuajiriwa kwa kazi maalum nchini Marekani, nyakati hizo alipokuwa mwana mitindo jijini New York, Mwandishi wa BBC,Gary O' Donoghue mjini Washington.