Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov amekiri kwamba uhusiano kati ya Moscow na Marekani umedorora sana.
Hata hivyo baada ya mkutano na mwenzake wa Marekani Rex Tillerson, bwana Lavrov amesema Urusi ilikua tayari kwa mazungumzo.

Waziri huyo amesema dunia inakua mahali bora ikiwa pande zote zitashirikiana na kuwa na sauti moja .
Na katika Umoja wa Mataifa, Urusi ilipiga kura ya turufu dhidi ya pendekezo kutaka Syria ishirikiane na uchunguzi kuhusu shambulio la silaha za kemikali.
Pendekezo hilo liliwasilishwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa.
Naibu balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vladimir Safronkov amesema pendekezo hilo linahalalisha shambulio la Marekani katika kambi ya wanahewa wa Syria wiki jana.