Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Apr 11, 2017

WATATU WAITWA MAREKANI KWA TUHUMA ZA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA

Waziri wa Katiba na Sheria amewasilisha maombi  ya kuwasafirisha washitakiwa watatu akiwemo Ally Hatibu Hassan maarufu kama Shkuba  kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kujibu tuhuma za kusafirishaji dawa za kulevya.

Washitakiwa wengine ambao wanaungana na Shkuba ni Idd Mafuru na Lwitiko Emmanuel Adam.
Maombi hayo yamewasilishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya kifungu namba 5 (1) cha Sheria ya Usafirishaji wahalifu sura ya 368 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Katika maombi hayo upande wa waziri kupitia DPP wanaiomba mahakama hiyo isikilize ushahidi na itoe amri ya kuwahifadhi washitakiwa ndani wakiwa wanasubiri kibali cha Waziri huyo cha kuwasafirisha nje ya nchi kwa mashitaka hayo
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP