Picha ya kwanza ya video ya watoto wa kiume waliokuwa wamekwama mapangoni huko nchini Thailand imeonekana,ikiwaonyesha watoto hao 12 na kocha wao wakiwa wanapatiwa matibabu.
Watoto kadhaa wanaonekana wakiwa wamefunikwa usoni isipokuwa mmoja tu anayeonyesha alama ya ushindi kupitia vidole vyake.

Nacho kikosi cha uaokoaji cha Thailand kimeonyesha video mpya inayoonyesha siku tatu za uokoaji,ambazo zimevuta hisia kwa watu waliowengi duniani.
Wazamiaji wanasema watoto hao walipewa dawa ya usingizi ili kuwaondolea hofu wakati wa uokoaji na walilazwa katika kitu kama kitanda maalumu.
Hata hivyo hadi sasa haifahamiki kama watoto hawa watafanikiwa kuhudhuria fainali za kombe la dunia siku ya jumapili kama walivyoalikwa na Rais FIFA.
Watoto wana michezo wakiwa hospitali
Image captionWatoto wana michezo wakiwa hospitali
Lakini operasheni hiyo ilisitishwa usiku ili mitungi ya hewa ya kusaidia kupumua ipate kujazwa.
Wakoaji waliamua kuendelea na oparesheni hiyo hatari kuwaokoa kufuatia hofu kuwa huenda maji yangeongezeka tena.
Mamilioni ya lita za maji yamekwisha kutolewa kutoka ndani ya pango hilo,ili kurahisisha kazi ya uokoaji.
Kazi hiyo inaharakishwa kufuatia utabiri wa hali ya hewa unaodai kwamba huenda mvua kubwa itanyesha jambo ambalo litasababisha ugumu wa kazi ya kuwaokoa watoto hao.
Kiongozi wa kikosi cha uokoaji ambaye gavana wa jimbo la Chang Raiu Narongsak Osottanakorn, amesema uokoaji huo wenye mazingira ya hatari utawachukua takribani siku nne kutegemeana na hali ya hewa, japo kuwa jana kwamba amesisitiza kila kitu kinaenda sawa.
Maafisa wa huduma za dharuraHaki miliki ya pichaAFP

Wavulana hao wanaondolewa kwa njia gani?

Kundi la wataalamu wa kupiga mbizi 90 kutoka Thailand na 50 kutoka nchi za kigeni wamekuwa wakifanya kazi kwenye pango hilo.
Wamekuwa wakiwaelekeza wavulana hao kwenye giza na maeneo yaliyofurika maji kwenda mlango wa pango.
Kufika mahala wavulana hao wapo na tena kufanya safari ya kurudi ni kazi ngumu hata kwa wapiga mbizi wenye ujuzi.
wavulana hao wakiwa kwenye picha ya pamoja na kocha wao
Image captionwavulana hao wakiwa kwenye picha ya pamoja na kocha wao
Shughuli hiyo inahitaji kutembea, kupanda na kupiga mbizi wakifuata kamba ambazo tayari zipo pangoni.
Akiwa amebeba vifaa vya hewa kila mvulana huandamana na wapiga mbizi wawili ambao pia hubeba hewa yake ya kupumua.
Wavulana hao wanaondolewa kwa njia gani?
Image captionWavulana hao wanaondolewa kwa njia gani?
Sehemu ngumu zaidi ya pango hilo ni ile inayoitwa T-Junction, ambayo ni nyembamba sana ambapo inawalazimu wapiga mbizi kuvua mitungi yao ya gesi ili waweze kupita.
Mbele ya hapo kuna sehemu inayojulikana kama Chamber 3.
Ni eneo wavulana hao hupumzika ili wapate kutembea kwenda kwa mlango wa pango. Hapo ndipo wao hutolewa na kupelekwa hospitalini huko Chiang Rai.
Pango
Image captionPango