Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika Kijiji cha Kisanga Kata
ya Kisanga wilaya ya Sikonge tarehe 12 Julai, 2018. Wengine wanaoshuhudia ni
Viongozi Waandamizi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Sikonge, REA, TANESCO,
Wakandarasi pamoja na wananchi.



NA
RHODA JAMES - SIKONGE
WAZIRI
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, jana tarehe 12 Julai, 2018   amewasha rasmi umeme  katika kijiji cha Kisanga kata ya Kisanga
wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora.
Waziri
Kalemani amewasha umeme huo baada ya kufanya uzinduzi wa mradi husika mwaka
jana wilayani Sikonge.
“Leo
nimekuja kuwasha umeme, kukagua utekelezaji wa mradi wa REA hapa Sikonge na
kuwakabizi Wakandarasi ili kumalizia vijiji vilivyobakia,” alisema Waziri
Kalemani.
Akizungumza
katika mkutano huo, Waziri Kalemani alisema kuwa Wilaya ya Sikonge ina jumla ya
vijiji 71 na hadi sasa vijiji 30 tayari vina umeme ingawa sio kikamilifu,
vijiji 40 vilivyobakia vyote vitapelekewa umeme.
Aliongeza
kuwa, mradi huu wa REA III awamu ya kwanza takriban vijiji 26 vitaletewa umeme,
vijiji 4 vipo off gridi kwa hiyo vitapatiwa umeme wa Jua (Solar) na vijiji
vingine 11 vilivyobakia vitaendelea kuunganishiwa umeme.
“Wakandarasi
hawa watawaletea umeme Kijiji kwa Kijiji, Kitongo kwa Kitongoji, Nyumba kwa
Nyumba bila kuruka nyumba yoyote” alisisitiza Waziri Kalemani.
Pia,
Waziri Kalemani aliendelea kuwahimiza Wafanyakazi wa Halmashauri kutenga pesa
kwa ajili ya kuunganishia umeme Taasisi zote za Umma.
Alisema
kuwa, ikiwa suala la kutenga pesa hiyo itakuwa ngumu basi, Ofisi zenye chumba
kimoja hadi vitatu wekeni kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho hakihitaji
wiring ili taasisi zote za umma zipate nishati hii ya umeme.
Aidha
kwa upande wake, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakuda ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Sikonge alimshukuru sana Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani
kwa ushirikiano mkubwa anaoendelea kumpa na kusema kuwa wananchi wa Sikonge
wanahitaji umeme ili kuendelea kufungua Viwanda vidogo vidogo na hata kuboresha
kipato cha kiuchumi katika miongoni mwao.




  Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akijiandaa kukata utepe na kuwasha umeme
katika Kijiji cha Kisanga. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph
Kakuda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge.


  Wananchi
wa kijiji cha Kisanga wakisalimia viongozi waliofika katika kijiji hicho.


  Kamishna
wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga akiwasalimia wananchi katika mkutano huo wa
kuwasha umeme katika kijiji cha Kisanga Kata ya Kisanga.




Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, Gidion Kaunda akiwasalimia wananchi
kabla ya zoezi la kuwasha umeme.