Yobnesh Yusuf ‘Batuli’
STAA wa sinema za Kibongo mwenye mvuto mbele ya kamera, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amevunja ukimya kwamba, kutoonekana kwake muda mrefu kwenye gemu ni moja ya njia za kuwapa hamu mashabiki wake ili wasimchoke, jambo ambalo limemletea heshima.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Batuli alisema alikaa kimya kwa muda mrefu kwa sababu kuna vitu alikuwa anaviweka sawa kisha arudi tena kwenye ulingo wa filamu na anashukuru Mungu
amevikamilisha.“Kutoonekana mara kwa mara kumeniletea heshima hata kwa mashabiki wangu. Kuonekana kila wakati inasababisha watu wanakuchoka, ni bora ukae kimya, ukiwa na kitu ndiyo unaibuka tena na ndivyo wanavyofanya hata wenzetu wa nje,” alisema Batuli.