MAAJABU YA DUNIA! Mwanamke Maurine Atieno, Raia wa Kenya amekamatwa na Jeshi la Polisi la Migori, nchini humo baada ya kuonekana akiishi na wanaume wawili Robert Ochieng na John Ochola ndani ya nyumba kimoja katika Kijiji cha Chamgiwadu.


Maurine amekamatwa na wanaume wake baada ya majirani kulalamikia kitendo cha jilani yao huyo kuishi na wanaume wawili kwa pamoja kinyume na mila na desturi zao. Inaelezwa kwamba, mama huyo amekuwa akiishi na waume wake hao ambao pia wamekamatwa ndani ya nyumba moja kwa wiki mbili sasa.

Mama huyo ambaye ni muuza samaki Mjini Kisumu Mjini anadaiwa anatuhumiwa kumlazimisha Ochola kuhamia nyumbani kwake na kuanza kuishi pamoja na Ochieng kwenye chumba hicho kimoja.

Mama wa Ochola amesema kwamba, muuza samaki huyo (Maurine) amekuwa kwenye mahusiano na mwanaye kwa muda mrefu na anamfahamu kama mke wa mwanaye lakini pia amekuwa akienda kuwatembelea nyumbani kwao na kijana huyo mara kwa mara.

Kwa mujibu wa chifu wa eneo hilo, amesema hakuna sheria inayoweza kutumika kuwashtaki ila wataangalia namna ya kuwatenganisha.